Heche ametoa kauli hiyo mchana wa leo ikiwa ni muda mfupi baada ya habari za Mkuu huyo wa Mkoa kusambaa akiweka wazi wilayani Mbulu kwamba hayuko tayari kutoa msaada kwa diwani wa chama cha upinzani kwa kuwa yeye anatekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani.
Heche amesema kutokana na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo mkubwa wa mkoa anasubiri kusikia kauli ya Chama chake na rais aliyemteua Mnyeti.
Aidha Mbunge huyo amesisitiza kwa kusema kwamba "Ubaguzi ni ubaguzi tu uwe wa rangi, kabila,dini au hata vyama".
Post a Comment