Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemwagiza katibu Mkuu wa Wizara
hiyo anayeshughulikia uvuvi Dk. Yohana Budeba pamoja na wakurugenzi
wote wa halmashauri za wilaya katika mikoa ya kanda ya
ziwa,
Kuwafuta kazi mara moja watumishi 65 na viongozi wa kamati za usimamizi
wa raslimali za uvuvi (BMU) 26 baada ya kubainika wanashiriki kufadhili
uvuvi haramu ndani ya ziwa Victoria.
Akihitimisha operesheni maalum ya kitaifa ya kupambana na kudhibiti
uvuvi na biasahara haramu ya mazao ya uvuvi katika ukanda wa Ziwa
Victoria iliyodumu kwa siku 40, katika ukumbi wa chuo cha benki kuu
jijini Mwanza, Mpina amesema operesheni hiyo itaendelea hadi disemba
mwaka huu ili kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa huku akidai hatasita
kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kukwamisha
juhudi za serikali.
Waziri Mpina pia ameonesha kuchukuzwa na kitendo cha askari wa
wanyamapori wa hifadhi ya kisiwa cha Lubodo mkoani geita kuwazuia
watendaji wa kikosi cha operesheni hiyo wakati wa msako dhidi ya uvuvi
haramu.
Operesheni hiyo ilianza Januari mosi mwaka huu, ambapo jumla ya wadau
1,200 waliopo kwenye sekta ya uvuvi nchini walikutwa na makosa
mbalimbali na kutozwa faini ya shilingi Bilioni 4.7, huku tani 73 za
samaki wasiokidhi kiwango wakigawiwa kwa wananchi,na tani 173 za mazao
ya uvuvi zilitaifishwa,huku mali na zana mbalimbali za uvuvi zenye
thamani kubwa ya fedha zikiteketezwa kwa moto.
WATUMISHI 91 KANDA YA ZIWA WAFUKUZWA KAZI SERIKALINI
Title: WATUMISHI 91 KANDA YA ZIWA WAFUKUZWA KAZI SERIKALINI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemwagiza katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia uvuvi Dk. Yohana Budeba pamoja na wakuruge...
Post a Comment