Mmoja wa viongha wapagazi wa chama cha wapagazi akizungumza na wanachama wa chama hicho |
Katibu wa Bodi ya TPO, Mussa Juma akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo na wanachama wa chama cha wapagazi waliohudhuria katika uchaguzi huo |
Baadhi ya wanachama wakisiliza kwa makini sera za wagombea waliokuwa wakijinadi na kuomba kura kwa wanachama hao |
Baadhi ya porters wakiwajibika kuwasaidia watalii katika mlima kilimanjaro |
baadhi ya porters wakiwa wamepumzika |
Mwandishi wetu, Moshi
Chama cha wapagazi wa Mlima Kilimanjaro(TPO), juzi kimechagua viongozi wapya, ambao wataongoza chama hicho kwa miaka mitatu.
Katika
uchaguzi huo, uliofanyika ukumbi cha Umoja hosteli mjini Moshi kwa
kusimamiwa na bodi ya chama hicho, Elibariki Sam alichaguliwa kuwa
Mwenyekiti.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo,ambao ulishirikisha viongozi kutoka kanda nne
za Marangu, Machame, Arusha na Moshi, Katibu wa Bodi ya TPO, Mussa Juma
jumla la kura zilizopigwa zilikuwa ni 19.
Alisema
Sam alipata kura 8 akifatiwa na Lotang'amwaki Mollel aliyepata kura 6,
Hemedi Juma kura 4 na kura mbili ziliharibika huu mgombea Frank Mpunju
akikosa kura baada ya kujitoa.
Juma alisema kwa mujibu wa taratibu cha TPO, Mollel alichaguliwa kushika nafasi ya makamu Mwenyekiti wa chama hicho.
Alisema
viongozi hao, wataungana na secretarieti ya TPO, ambayo inaongozwa na
Katibu Mtendaji Loshiye Mollel na viongozi wa wengine kutoka kanda ya
Arusha, Marangu, Machame na Moshi.
Akifungua
mkutano huo, Mwenyekiti wa bodi wa chama hicho, Alex Lemunge aliwataka
wapagazi kujiendeleza kielimu na ambao watashindwa watakuwa wanajiondoa
kufanyakazi hiyo.
Lemunge
alisema, utaratibu wa kujiendeleza kielimu, umetolewa na wizara ya
maliasili na Utalii, ili kuhakikisha watoa huduma wote kwa watalii
wanakuwa na elimu na kusajiliwa.
Alisema
tayari utaratibu wa kusoma umeanza kuwekwa baina ya TPO kwa
kushirikiana na chuo cha Wanyamapori cha Mweka na wadau wengine,
kuhakikisha wapagazi zaidi ya 20,000 wanapatiwa elimu juu ya kazi zao
ili kupata sifa ya kufanyakazi hiyo.
Post a Comment