PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SERIKALI AFRIKA MASHARIKI ZATAKIWA KUONDOA VIKWAZO VYA AJIRA WAFANYAKAZI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkutano Mkuu wa Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha Msajili wa vyama vya wafanyakazi Nchini TANZANIA Bi. Pe...



Mkutano Mkuu wa Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha


Msajili wa vyama vya wafanyakazi Nchini TANZANIA Bi. Pendo Zacharia Berege akizungumza KATIKA Mkutano WA mwaka WA Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki 


MAKAMU mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki Dokta Francis Atwol akizungumza KATIKA Mkutano Mkuu wa Mwaka WA Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki Jijini Arusha mapema leo


Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyakazi nchini Tanzania (Tucta) Ndugu Henry Mkonda akiwakaribisha viongozi wa mashirikisho ya wafanyakazi WA Nchi za Afrika Mashariki katika mkutano Mkuu wa Mwaka WA Shirikisho la Wafanyakazi Afrika Mashariki Jijini Arusha mapema leo


Na: Andrea Ngobole, Arusha



 Shirikisho la wafanyakazi Afrika ya Mashariki(EACTC) limeomba serikali za Afrika ya Mashariki kuondoa vikwazo kwa utoaji vibali vya ajira kwa wafanyakazi wanaohama kutoka nchi moja hadi nyingine.


Kwa mujibu wa itifaki ya Soko la Pamoja katika Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wafanyakazi baina ya nchi wanachama wanaweza kufanyakazi katika nchi wanachama bila ya vikwazo baada ya kufuata sheria za kila nchi mwanachama.



Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la wafanyakazi Afrika Mashariki Dk.Francis Atwoli akizungunza katika mkutano wa mwaka wa EACTC jijini Arusha Leo amesema bado Kuna changamoto ya utolewaji WA vibali vya kazi baina ya Nchi Wanachama WA jumuiya hiyo.


Atwoli alisema  itapendeza mfanyakazi wa Tanzania Akiwa na sifa aweze kufanya kazi nchi  nyingine Kama Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi bila vikwazo.


 Dk Atwoli amempngeza  Rais was Tanzania  Samia  Suluhu Hassan kwa kujali wafanyakazi kwa kupandisha mishahara kwa wafanyakazi na kuwaomba maraisi wengine kuiga na kuheshimu sheria za kimataifa za kazi.


Msajili wa vyama vya wafanyakazi nchini, Pendo Berege alisema  vyama vya wafanyakazi  EAC vinapaswa kujenga mfumo wa majadiliano na waajiri kuliko kugoma kufanya kazi kwani haileti tija kazini na matokeo yake Huwa si mazuri.


Hata hivyo  alisema kwa Sasa kuna  utulivu mkubwa kwa vyama vya wafanyakazi nchini Tanzania kwani vinazingatia kanuni na taratibu katika kutetea haki za wafanyakazi.


Awali Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini( Tucta )Henry Mkonda alisema ni vema vyama vya wafanyakazi EAC  kuwa pamoja katika kutatua changamoto za wafanyakazi.


"Muhimu kuwa na sauti moja katika kutetea haki za wafanyakazi na kufikia lengo linalotambua na kusimami sheria za kazi kwa kila nchi"alisema



Viongozi wa wafanyakazi Afrika Mashariki wanakutana Arusha kwa muda wa siku mbili katika mkutano unaowezeshwa na shirika la kazi Duniani (ILO)  ili kutatua kero za wafanyakazi.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top