PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TANROADS KUONGEZA ALAMA ZA WANYAMA ALIPOPATIA AJALI WAZIRI KIGWANGALA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  mwandishi wetu, Babati.   Wakala wa barabara(TANROADS) mkoa wa Manyara, imetangaza mkakati wa kuongeza alama za barabarani ka...

 Related image

Image result for picha za ajali ya kigwangalla
mwandishi wetu, Babati.
 
Wakala wa barabara(TANROADS) mkoa wa Manyara, imetangaza mkakati wa kuongeza alama za barabarani katika eneo la mapito ya wanyama kutoka minjingu hadi Mdori.

Akizungumza na wanahabari,Meneja wa TANROADS, mkoa wa Manyara Mhandisi, Bashiri Rwesingisa, alisema wameamua kuongeza alama za barabarani katika eneo hilo ili kupunguza ajali za binaadamu na vifo vya wanyamapori.

"lile eneo pale hatuwezi kuweka matuta ila tutaongeza alama za wanyama kwani ni ukweli kuwa ajali zinatokana na wanyama kuvuka katika eneo hilo ambalo lina msitu"alisema

Alisema miongoni mwa alama ambazo zitaongezwa ni michoro na mabango ambavyo vitaonesha eneo hilo lina idadi kubwa ya wanyamapori hivyo, dereva achukuwe tahadhari.

Rwesingisa alisema TANROADs ipo tayari kushirikiana na wadau wa usalama barabarani na wadau wa utalii, ili kuhakikisha ajali za magari na wanyama zinapungua katika eneo hilo lenye kilomita 13.

Awali Meneja wa kampuni ya Chem chem,Charles Silivester na Mwenyekiti wa jumuiya ya uhifadhi wanyamapori ya  burunge(WMA),Ismail Ramadhani walishauri eneo hilo kuwekwa matuta.

Silivester alisema katika eneo hilo, kwa wiki moja wanyama wasiopungua wanne ugonjwa hasa kutokana na mwendokasi wa madereva licha ya kuwepo alama za wanyama.

"sisi baada kuona ajali zinaongezeka na hii ya juzi ya waziri tuliomba matuta na chemchem tupo tayari kushirikiana na TANROADS kupunguza hili tatizo"alisema

Kwa upande wake, Ramadhani alisema, jumuiya yao inasikitishwa na matukio ya ajali katika eneo hilo na wanaamini linachangiwa na vitu vingi, ikiwepo uvamizi wa watu katika maeneo ya mapito ya wanyama.

"tunataka serikali ichukuwe hatua kulinda haya mapito sisi kama WMA tunafanya kazi kubwa kulinda wanyama na sasa wameongezeka lakini uvamizi wa shughuli za binaadamu umekuwa mkubwa"alisema

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla Augost 4, alipata ajali katika eneo hilo, wakati gari alilokuwa amepanda kumkwepa Twiga na katika ajali hiyo, afisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba alifariki na wengine wawili kujeruhiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top