PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TAASISI YA FRIEDKIN CONSERVATION FUND YATOA SHILINGI MILION 110 KUSAIDIA ELIMU SIMIYU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Wakurugenzi wa taasisi ya friedkin conservation fund wakiongozwa na Abdukadir Mohamed wakikabidhi hundi ya shilingi milioni 110 kwa mkuu...
 Wakurugenzi wa taasisi ya friedkin conservation fund wakiongozwa na Abdukadir Mohamed wakikabidhi hundi ya shilingi milioni 110 kwa mkuu wa mkoa wa Simiyu Bwana Anthony Mtaka kwa ajili ya kusaidia elimu katika mkoa huo ambapo hafla ilifanyika katika uwanja wa Maonesho ya Nanenane Nyakabindi wilaya ya Bariadi

Baadhi ya wananchi wakiwa katika banda la fiedkin conservation fund wakijiona miradi mbalimbali iliyokwisha tekelezwa na mfuko huo

Picha ya pamoja ya wakurugenzi wa friedkin conservation fund
 

Mwandishi wetu, Simiyu.

Taasisi ya uhifadhi na Utalii ya friedkin Conservation Fund,imetoa msaada ya sh 110 million ili kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari ya vipaji maalum mkoa wa Simiyu.

Msaada huo,ulikabidhiwa Jana kwa mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na  wakurugenzi wa taasisi hiyo wakiongozwa na Abdukadir Mohamed katika hafla iliyofanyika uwanja wa Maonesho ya Nanenane Nyakabindi wilaya ya Bariadi.

Mohammad  alisema Taasisi yao ambayo inamiliki kampuni za Uwindaji na upigaji picha za  Kitalii,Mwiba holdings  Ltd na Tanzania Game Trackers Safaris, ambazo zimewekeza mkoani humo,zimetoa msaada huo kusaidia watoto kupata elimu.

Alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ya kusaidia jamii inayotolewa ili kuchangia maendeleo  ya mkoa wa Simiyu.

"Tunachoomba ni kupewa ushirikiano tufanye kazi zetu za utalii katika pori la akiba la Makao na Maswa na kuondolewa uvamizi " alisema

Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alishukuru msaada huo wa sh 110 milioni ambazo zitasaidia ujenzi wa shule hiyo.

Alisema Taasisi ya Friedkin imekuwa na mchango mkubwa wa maendeleo  katika mkoa huo kwani hivi karibuni ilitoa msaada ya mifuko 3000 ya saruji na bati 1000 kusaidia elimu.

Alisema licha ya msaada huo,taasisi hiyo imesaidia kutoa ajira,inalipa kodi na imekuwa ikilipa kodi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Meatu Dk Joseph Chilongani alisema serikali inatambua mchango wa taasisi hiyo kwa maendeleo  ya jamii.

Alisema licha ya misaada  inayotolewa ngazi ya mkoa Taasisi hiyo kila mwaka inatoa zaidi ya sh 610 milioni kama kodi ya pango na sehemu ya mapato ya utalii kwa vijiji 10 vilivyopo eneo la hifadhi ya jamii ya makao.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM(NEC) mkoa wa Simiyu Gungu Silanga alisema serikali ya CCM itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo kwani inachangia utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi.

"Miaka ya nyuma kulikuwa na watu wachache walitaka kutogombanisha lakini sasa chama na serikali tupo pamoja kufanya kazi na wawekezaji mkoa wa Simiyu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Merkur - The merit casino
    The Merkur 933 is a 6,3-inch 카지노사이트 HD The Merkur 933's razor offers a solid head with a unique angle งานออนไลน์ that allows the razor deccasino blade to be

    ReplyDelete

 
Top