Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za maadhimisho
ya 25 ya Nanenane kwa mwaka 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi,
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 3 Agosti
2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Waziri
wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza kilimo cha vitunguu vidogo
ambavyo soko lake ni kubwa kuliko vitunguu vidogo mara baada ya
kutembelea Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwenye sherehe za maadhimisho
ya 25 ya Nanenane kwa mwaka 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi,
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 3 Agosti
2018.
Mgeni rasmi-Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Mhe Antony Mtaka Mkuu wa Mkoa mwenyeji wa sherehe za maadhimisho
ya Nanenane kwa mwaka 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi, Halmashauri
ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wakitembelea mabanda mbalimbali jana
tarehe 3 Agosti 2018.
Mgeni
rasmi-Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati
akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za maadhimisho
ya 25 ya Nanenane kwa mwaka 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi,
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 3 Agosti
2018.
Mgeni
rasmi-Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akipiga ngoma ya asili ya
kabila la kisukuma ishara ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho
ya 25 ya Nanenane Kitaifa kwa mwaka 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi,
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu jana tarehe 3 Agosti
2018. Wengine pichani (Kulia) ni Katibu Mkuu wizara ya mifugo na Uvuvi
Prof Elisante Ole Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe Adam Malima, Ndg
Enock Yakobo na Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Ndg Jumanne
Sagini, Naibu waziri wa kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa, Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe Antony Mtaka na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah
Ulega.
Na Mathias Canal, WK-Simiyu
Waziri
wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, jana 3 Agosti 2018 amezindua
maadhimisho ya 25 ya Nanenane kwa mwaka 2018 katika Viwanja vya
Nyakabindi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu huku akitoa
wito kwa wananchi wote wa mikoa inayounda
kanda ya Ziwa Mashariki ambayo inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na
Shinyanga kutumia fursa ya kutembelea katika maonesho hayo ili kujifunza
mbinu mbalimbali za kitaalamu katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Akizungumza
na mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa maonesho hayo Dkt
Tizeba aliwasihi wananchi wote kutumia fursa ya maonesho hayo kwa
kuwatumia ipasavyo wataalamu ambao watakuwepo katika viwanja hivyo kwa
siku zote za maonesho hayo ili kupata ushauri na maelekezo ya kuboresha
shughuli zao za kiuchumi kupitia Kilimo, Ufugaji, Uvuvi na Ushirika.
Alisema
kuwa wananchi wanapaswa kutembelea katika maonesho hayo kwa lengo la
kujifunza ili kuwa tayari kuanza kutumia teknolojia na maarifa
watakayopata kwa lengo la kujiletea mapinduzi halisi katika kilimo,
mifugo na uvuvi.
Mhe
waziri Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini itaendelea kuwa sekta
muhimu katika maendeleo ya uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla
hususani katika wakati huu ambapo serikali imejidhatiti kufikia uchumi
wa viwanda. Alisema sekta ya kilimo imeendelea kuimarika kwa kuchangia
Pato la Taifa hadi asilimia 30.1 kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na
asilimia 29.2 mwaka 2016.
Sambamba
na hayo Mhe Tizeba alisema kuwa ushirika ni sekta mtambuka inayohusisha
sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Madini, Viwand,
Nyumba na Fedha (Ushirika wa Akiba, Mikopo na Benki) ambazo zinagusa
wananchi wengi zaidi.
Alisema
kutokana na umuhimu wa sekta hiyo, Wizara kupitia Tume ya maendeleo ya
ushirika imeendelea kuwezesha na kuimarisha ushirika ili wananchi waweze
kunufaika na fursa zinazopatikana katika ushirika kwa lengo la
kuchangia katika kuongeza kipato kwa wananchi wengi hususani waliopo
vijijini.
Alisema
katika mwaka 2017/2018, Tume imefanya uhamasishaji wa wananchi kujiunga
au kuanzisha vyama vya ushirika ambapo hadi kufikia Disemba 2017 vyama
vipya 394 vilisajiliwa na kufanya idadi ya vyama vya ushirika kufikia
10,990 kutoka 10,596 vilivyokuwepo Machi 2017.
Alisema
vyama hivyo vinakadiriwa kutoa ajira mpya kwa wananchi takribani 1,182
huku katika kipindi cha mwaka 2017/2018 wanachama wapya 385,295
walijiunga au kuanzisha vyama vya ushirika na kufanya idadi ya wanachama
kuongezeka kutoka 2,234,016 hadi kufikia 2,619,311
Post a Comment