Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu ,Profesa Joyce Ndalichako akifungua mkutano huo |
Washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Waziri, Professa Joyce Ndalichako |
Mshauri wa masula ya kiufudi wa shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa(ILO) katika ukanda wa Kusini mwa Afrika,Gloria Moreno Fontes akizungumza na waandishi katika mkutano wa uhamaji ajira. |
Na: Andrea Ngobole, Arusha
Shirika la Kimataifa la Kazi Duniani(ILO) limetaka watendaji katika utatu wa uhamaji nguvu Kazi na usimamizi uhamiaji kufanya Kazi kwa ushirikiano ili kuwezesha wafanyakazi kufanya Kazi kutoka nchi moja hadi nyingine.
Mshauri wa masula ya kiufudi wa shirika la Kazi la kimataifa(ILO) katika ukanda wa Kusini mwa Afrika,Gloria Moreno Fontes akizungumza katika kikao Kazi cha wataalam vyama vya wafanyakazi, maafisa uhamiaji na idara za Kazi pamoja na waajiri alishauri uwepo ushirikiano baina yao.
Moreno amesema shirika hilo linawajengea uwezo vyama vya waajiri,Taasisi za serikali na vyama vya wafanyakazi ili kuondoa changamoto za uhamaji nguvu kazi kutoka nchi moja hadi nyingine.
"ILO itaendelea kusaidia Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi zilizo katika mradi wa kuboresha Mazingira ya uhamaji nguvu kazi na masuala ya uhamiaji"amesema
Akifungua mkutano huo,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu ,Profess Joyce Ndalichako amesema mkutano huo utawezesha usimamizi mzuri wa utatu wa uhamaji wa nguvu kazi na usimamiaji uhamiaji kutoka nchi moja hadi nyingine.
Waziri Ndalichako alisema changamoto za wafanyakazi nje ya nchi zinaweza kupatiwa Suluhu Kama utatu huo ukifanyakazi vizuri.
" Tumekuwa tukiona wafanyakazi wanapopata shida ndipo wanakimbilia Ofisi za ubalozi lakini walipaswa kufuata sheria na taratibu wanapokwenda kufanyakazi"amesema
Profesa Ndalichako, amesema uhamaji nguvu kazi kutoka nchi moja hadi nyingine unapaswa kuzingatia Sheria na mikataba ya kimataifa.
Alisema mradi huo wa uhamaji nguvu pia unatekekezwa na nchi nyingine ambazo ni Kenya, Ethiopia,Uganda na Sudani Kusini .
Ofisa ofisi ya Kamishna wa Kazi Zanzibar Amir Ally Amir alipongeza uwepo was mradi huo ambao utapunguza kero za wafanyakazi.
Post a Comment