Vijana wasomi na wajasiriamali nchini, wametakiwa kwenda vijijini
kubuni miradi midogo midogo ya maendeleo, kutokana na kuimarika
upatikanaji wa nishati ya umeme vijijini na ili waweze kujiletea
maendeleo .
Ushauri
huu umetolewa jijini Arusha katika mafunzo kwa vijana kutoka maeneo
mbalimbali ya nchi mafunzo ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Energe
Change Lab kwa udhamini wa mashirika ya kimataifa ya Hivos na iied , jijini Arusha.
Akitoa
mada katika mafunzo hayo, Lilian Madege akisema upatikanaji wa umeme
vijijini unapaswa utumike kama fursa kwa vijana kubuni miradi midogo
ambayo hapo awali ilikuwa ni vigumu kutekelezeka kutokana na kutokuwepo
na huduma ya umeme wa uhakika.
Madege
alisema Tanzania kwa sasa upatikanaji umeme katika maeneo mengi
unaridhisha hivyo, badala umeme huo kutumika majumbani pekee unapaswa
kuwa fursa kwa vijana vijijini kuwa na miradi ya maendeleo.
Akizungumza
kwenye mafunzo hayo, Filomena Philipo ambaye ni mjasiliamali mdogo
alisema kuwa , mtandao wa upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo
ya vijijini kumechagiza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya vijana lakini
bado kuna changamoto ya ukosefu wa mafunzo kwa vijana ni kwa jinsi
gani wanaweza kutumia nishati hiyo kwa upana zaidi.
"tunaomba
mafunzo zaidi kwa wajasiriamali vijijini ili kuweza kutumia umeme kama
moja ya fursa za kiuchumi hivyo mradi kama huu Energ Safari unapaswa
kuendelezwa"alisema
Katika
mradi huo kwa kutambua fursa zitokanazo na umeme, ambao unafadhiliwa na
mashirika ya kimataifa ya Hivs na iied vijana walioshiriki walipata
fursa ya kutembelea vijiji kadhaa mkoani Arusha na kuona fursa
zinazoatikana na pia changamoto ambazo zinazuia umeme kutumika katika
miradi midogo kwa vijana.
Post a Comment