Mwenyekiti
wa HoneyGuide Foundation Olekiri Mbai akikabidhi gari aina ya Suzuki
Jimmy kwa Mkuu wa Wilaya wa Monduli Iddi Hassan ikiwa ni msaada wa
shirika hilo katika kusaidia hifadhi ya wanyamapori ya Randilen
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Hifadhi
ya Wanyamapori ya Randlen Community Wildlife Management iliyoko
wilayani Monduli imekabidhiwa gari aina ya Suzuki Jimmy kwa ajili ya
kudhibiti vitendo vya ujangili na uharibifu wa mazingira katika hifadhi
hiyo ya jamii .
Akipokea
gari hilo kutoka Shirika la Honey Guide Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi
Hassan alisema kuwa gari hilo litasaidia juhudi za kupambana na ujangili
katika wilaya hiyo ambayo ili kukuza utalii endelevu kwa manufaa ya
jamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu
wa Wilaya hiyo amesema kuwa msaada huo utasaidia kuimarisha shughuli za
uhifadhi kwani hifadhi hiyo ni hifadhi pekee inayofanya vizuri katika
wilaya hiyo na kunufaisha vijiji tisa vinavyozunguka hifadhi hiyo.
Iddi
alisema kuwa kwasasa wanajipanga katika kuzuia uvunaji holela wa
maliasili katika hifadhi pamoja na kuzuia ujangili hivyo msaada huo wa
gari utaongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ujangili.
Mwenyekiti
wa Honey Guide Foundation Olekiri Mbai amesema kuwa wameamua kutoa
msaada huo unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 25 ili kusaidia
shughuli za uendeshaji wa hifadhi hiyo ya jamii (WMA) katika kuunga
mkono juhudi za serikali kuhakikisha kuwa uhifadhi unafanyika kwa namna
ambayo unanufaisha wanajamii wa Monduli.
“Kumekua
na changamoto ya Hifadhi nyingi kutokuwa na Meneja lakini hifadhi ya
Randilen ni hifadhi pekee yenye meneja ambaye anasimamia shughuli zote
za utawala hivyo msaada huu wa gari utamsaidia kutekeleza majukumu yake
ya kila siku” Alisema Olekiri
Mwenyekiti
wa Hifadhi hiyo Daniel Alais ameshukuru shirika la Honey Guide kwa
kutoa msaada huo ambao utasaidia kuongeza nguvu katika mapambano dhidi
ya ujangili na uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kurahisisha
utendaji kazi wa kila siku.
Post a Comment