Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Monduli Rose Mhina akifafanua jambo katika uzinduzi wa jukwaa la Uweshaji wa Wanawake kiuchumi.Picha na Ferdinand Shayo |
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Hassan akizungumza katika uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake Kiuchumi Ambalo lilihudhuriwa na wanawake kutoka kila kata ya Wilaya hiyo.Picha na Ferdinand Shayo |
Viongozi wa Wilaya wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wakiwa kwenye mkutano.Picha na Ferdinand Shayo |
Baadhi ya Wanawake kutoka wilaya ya Monduli wakifuatilia kwa makini mkutano.Picha na Ferdinand Shayo |
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Wilaya ya
Monduli imezindua rasmi jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo jukwaa
hilo linatarajia kusaidia vikundi vya kinamama vyenye uelekeo wa Ushirika
ikiwemo Vikundi vya uzalishaji mali,ujasiriamali pamoja na Vikoba.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Jukwaa hilo Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Hassan alisema
kuwa serikali ina jukumu la kuwawezesha wanawake kwa kupitia fedha zinazotengwa
na halmashauri kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya kinamama ili waweze kuinuka
kiuchumi.
Iddi
amewataka Wanawake hao kuzalisha bidhaa bora pamoja na kuzifungasha vyema ili
waweze kupata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.
Afisa ustawi
wa Jamii Wilaya ya Monduli Rose Mhina amesema kuwa jukwaa la Uwezeshaji wa Wanawake
litawasaidia wajasiriamali na vikundi vidogo vidogo ikiwemo VIKOBA katika
kuunganisha nguvu kwa pamoja na kutumia fursa ya kukopa fedha ili kujiendeleza
kiuchumi.
“Tumefanya uchaguzi
na kupata wawakilishi kila kata itatusaidia kufuatilia kwa karibu na
kuhamasisha masuala ya uwezeshaji wa wanawake kwa urahisi ili kuwafikia
wanawake wote katika wilaya ya Monduli” Alisema Rose
Mwenyekiti
wa Baraza la Uwezeshaji wa Wanawake mkoa wa Arusha Roda Msemwa alisema kuwa Jukwaa hilo lina
jukumu ya kuhamasisha shughuli za uzalishaji pamoja namna ya kuwawezesha
kiuchumi ili waweze kuondokana na umasikini katika kaya zao.
Post a Comment