Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas akiwasilisha
mada kuhusu majukumu ya vyombo vya habari katika sekta ya utalii kwa
wahariri na wanahabari waandamizi katika mkutano wa sita ulioandaliwa na
Hifadhi za Taifa (TANAPA) mkoani Tanga.
VYOMBO vya habari nchini havipaswi kuandika
mambo ambayo yanaweza kuathiri utalii wa Tanzania na badalayake vinapaswa kuwa
chachu ya kukuza na kuutangaza utalii.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk.
Hassan Abbas, amesema wanahabari wanapaswa kuhakikisha wanaandika mambo ambayo
yataweza kuwavutia watalii kuja nchini na kutembelea vivutio mbalimbali hatua
ambayo itasaidia kukuza pato la taifa.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada ya wajibu
wa vyombo vya habari katika sekta ya utalii kwenye mkutano wa wahariri na
wanahabari waandamizi wa kujadili sekta ya utalii nchini unaoendelea jijini
Tanga.
"Tunaweza kutumia vyombo vyetu vya habari
kuandika vizuri habari za utalii na sekta nzima ya utalii, kwa mfano Kenya
huwezi ukakuta wanaandika jambo ambalo wanaona linaweza kuiathiri nchi
yao," amesema Dk Abbas.
Dkt.Abbas
amewataka Wanahabari kuandika habari za Utalii kwa wingi katika suala
zima la kuutangaza Utalii wa nchi yetu,ambao ukitangazwa vizuri
itasaidia kukuza uchumi wetu na hatimae kuongeza pato la Taifa,akaongeza
kuwa pia na jamii inayozunguka katika suala zima la utalii itanufaika
kwa namna moja ama nyingine
"Tuwafadhili
Waandishi wa habari kufanya stadi muhimu kama habari za Takwimu (data
Journalism) na za uchunguzi (investigative journalism) kwa habari zenye
maslahi kwa Taifa kama vile kufichua mitandao ya Waharifu wa mazingira
au Majangili",alisema Dkt Abbas.
Waandishi
mbalimbali wa habari nchini wakisikilza mada wakati wa mkutano wa
Hifadhi za Taifa, Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi nchini
unaofanyika jijini Tanga.
Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas akiwasilisha mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza
kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli
mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. .
Pichani
kati ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC),Dkt
Ayub Rioba akiwa sambamba na Meneja Mahusiano wa TANAPA,Pascal Shelutete
na wadau wengine wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas alipokuwa akiwasilisha mada katika Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza
kufanyika jana kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga ,ambapo kauli
mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri ,Theophil Makunga akiwa na Wajumbe wengine
katika Mkutano wa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioandaliwa na
Tanapa
Wahariri
na Waandishi waandamizi wa Habari walioshiriki katika Mkutano Maalum wa
Mwaka ulioandaliwa TANAPA juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda
Mwandishi
wa gazeti la Mwananchi Mkoa wa Morogoro Lilian Lucas akipitia jarida
la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakati somo la umuhimu wa
kuhifadhi na kutangaza utalii wa eneo hilo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda akichangia jambo kwenye mada iliyohusu Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini, wakati wa mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ,Theophil Makunga akiuliza moja ya swali kwenye mada iliyohusu Wajibu wa Wanahabari katika kutangaza Utalii nchini,katika mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari Waandamizi juu ya Utalii na Tanzania ya Viwanda.
Post a Comment