MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Utangazaji (TBC),
Dk. Ayoub Rioba amesema chaneli ya utalii itakayokuwa ikirushwa na televisheni
hiyo itazinduliwa Desemba 30, mwaka huu.
Amesema chaneli hiyo itasaidia kukuza sekta ya
utalii nchini kwa kuwa kila Mtanzania pamoja na wageni wengine wataweza
kufahamu sekta ya utalii ya Tanzania kupitia chaneli hiyo.
"Tunatarajia kumaliza andiko Agosti 10
ambalo litaenda sambasamba na uombaji wa leseni ambao tunatarajia itakuwa
Septemba 10," amesema Dk Rioba wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa
wahariri na wanahabari waandamizi wa masuala ya utalii unaofanyika mkoabi Tanga.
Mratibu wa Mradi wa
Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa kutokana na Ukataji na Uharibifu wa
Misitu (MKUHUMI), Gerald Kamwenda akiwasilisha mada kuhusu hifadhi za
mazingira asilia na mikakati ya utalii kwa wanahabari.
Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah akifuatilia mkutano huo unaoendelea na mkoani Tanga
Waandishi
mbalimbali wa habari nchini wakisikilza mada wakati wa mkutano wa
Hifadhi za Taifa, Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi nchini
unaofanyika jijini Tanga.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.