Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) imesema kuwa ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa
fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74
Richard Kayombo - Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi (TRA)
Taarifa
iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi Bw.
Richard Kayombo imesema kuwa katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa
fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Desemba 2016, TRA imekusanya kodi
jumla ya shilingi trlioni 7.27 ikilinganishwa na kipindi kama hicho
mwaka wa fedha 2015/16.
Mlinganisho wa makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 uko kama ifuatavyo:
Kayombo amesema mambo yaliyochangia
ongezeko hilo ni pamoja na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza
maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kuziba
mianya ya upotevu wa mapato, pamoja na kuhimiza na kufuatilia matumizi
ya mashine za kielektroniki pamoja na ukusanyaji wa kodi za majengo.
Pia amewataka wafanyabiashara kuwasilisha ritani zao za VAT kabla ya tarehe 20 kila mwezi kwa mujibu wa sheria.
Post a Comment