Rapa Fid Q amefunguka na
kusema kuwa watu hawatakiwi kutishwa na msanii mwenye followers wengi
kwenye mitandao ya kijamii wakidhani kuwa mtu huyo ndiyo maarufu sana au
ndiyo kusema anakuwa na biashara sana kwenye soko la muziki.
Fid Q
Fid
Q aliyasema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusema wapo baadhi
ya wasanii ambao hawana watu wengi kwenye mitandao ya kijamii lakini ni
wasanii wakubwa na wanaweza kufanya show zao wenyewe na wakajaza na
makampuni makubwa yakawekeza pesa zao.
"Views za Youtube hazi'define' muziki
kufika kwa watu, nina ushahidi wa muziki ambao una views nyingi youtube
lakini watu hawaujui, Chameleone anaweza kufanya event hapa Tanzania na
ikawa na sponsors, ikajaza watu mpaka sponsors wakaweka hela zao na
hatokei hapa Bongo, sasa jiulize kwanini huyu ana followers wachache
kwenye mitandao ya kijamii au ana views chache youtube lakini ana soko
kubwa. Kuna watu ni maarufu mitandaoni lakini hawajulikani Mpitimbi hapo
au Nanjirinji hakuna mtu anawajua lakini ukienda kucheki followers
Instgram utakimbia" alisisitiza Fid Q
Kutokana na hilo Fid Q anawataka watu
kutodanganyika na maisha ya social networks akisema kuwa kuna maisha
yenye uhalisia nje ya mitandao ya kijamii
"Kuna wasanii wengine wana followers
wengi lakini wakifanya show wanachezea za uso, sasa hao followers
wanaishi wapi? Ina maana followers wengi ni feki? Hata kama wakiwa real
wengi hawa exist katika real life, sababu mtu kama una followers milioni
mbili unafanya event masaa haijazi hao followers wako wako wapi?
Alimaliza Fid Q
Post a Comment