NA ANDREA NGOBOLE, PMT
Swali moja kubwa linalowasumbua wanasosholojia na wataalam
wa uchumi ni kwa nini maskini wanaendelea kuwa maskini na matajiri wanaendelea
kuwa matajiri vizazi na vizazi vyao vyote?
Swali hili ni gumu kidogo kulipatia jibu makini kama
utafikiria kwa uchache ila ukweli ni kwamba umaskini na utajiri wote unatokana
na fikra zilizopo mwa mhusika mwenyewe wa namna ya kuweza kuwa tajiri na au
kuendelea kuwa maskini katika maisha yake na vizazi vyake vyote.
Kutokana na fikra hizo zilizojengeka akilini mwake na
hujikuta mtoto wake naye hurithi fikra hizo kwa sababu ya jinsi anavyoongea
naye, unakuta mzazi anakaa na mwanaye hukiri umaskini wake na kuona kama wao na
uzazi wao walizaliwa ili wawe maskini kitu ambacho mimi binafsi sikubaliani
nacho hata kidogo kwa sababu ambazo nitaziainisha baadae kidogo katika Makala hii.
Baada ya wanasosholojia kukaa na kufikiria sana juu ya
namana ya kuweza kukomboa jamii maskini walijiuliza maswali haya yafuatayo
Maswali haya na mengine mengi yaliwalazimu kufanya utafiti
wa sayansi ya jamii huko bara asia ili waje na majibu sahihi ya sababu haswa
zinazofanya jamii maskini kuwa maskini
Waliamua kumtafuta mtu maskini kabisa asiyekuwa na kitu wakawa
wanamfuatilia maisha yake kwa siku kadhaa wakaona kuwa ni maskini na maisha yake ni ya chini sana wakamtegeshea mfuko wenye
pesa nyingi sana kama milioni mia hivi za kitanzania na wakahakikisha yeye ndio
anaziokota pesa zile basi wakaanza kumfuatilia wajue atafanyia nini hizo pesa?
Maskini huyo alipookota hizo pesa alifanya yafuataayo
Baada ya miezi miwili pesa zote zikawa zimeisha na kurejea
katika maisha yake ya awali ya umaskini mkubwa usioelezeka tena Zaidi ya awali
alivyokuwa
Baada ya kupata
majibu hayo watafiti hao wakaja na jibu moja kubwa na kusema sababu inayowafanya maskini
kuendelea kuwa maskini ni kutokuwa na mawazo mazuri
yatakayowaingizia pesa za kila siku
Wakashauri pia kila mwananchi afundishwe utawala wa fedha na
mbinu za ujasiriamali ndio maana kwa sasa bara la asia ni moja ya mabara
yanayokuja juu sana klatika kujikwamua kiuchumi ngazi ya familia na taifa kwa
ujumla ndio maaana wahindi ni moja ya jamii toka barani Asia iliyosambaa dunia
nzima wakijihusisha na biashara mfano kwa hapa Tanzania wapo wengi na wanaongoza
kwa biashara pengine kuliko sisi wazawa ukienda mataifa ya marekani, Canada na uingereza
kote huko utawakuta wanafanya biashara na wameushikiilia uchumi wa mataifa
hayo.
Sasa ili uweze kuepukana na umaskini wa kipato lazima
ukubali pia kubadilika kifikra na kiuchumi lazima uwe na nidhamu ya kutumia
pesa yako kulingana na kipato chako yaani usitumie Zaidi ya unachokipata,
lazima uepuke vitu vya anasa, lazima ujiweke lengo la kuwa tajiri na sio kuonekana
tajiri, lazima uepuke starehe zisizo kuwa za lazima, lazima upende kujifunza
mbinu za ujasiriamali toka kwa wafanyabiashara waliofanikiwa pia ukipata nafasi
hudhuria semina za ujasiriamali ujifunze Zaidi lakini pia kutengeneza mtandao
na watu waliofanikiwa
Matajiri wengi wanapenda kurithisha watoto wao utajiri na huwafundisha mbinu za jinsi ya kuwa na
kuendelea kuwa tajiri, huwaelekeza namna ya kuwa na nidhamu ya pesa, huwafunza
matumizi ya pesa katika mgawanyo wa asilimia ambao nilishaueleza katika Makala iliyopita
ya FANYA KAZI KWA BIDII ILI UUKIMBIE UMASKINI, huwapa mbinu mbalimbali za kubuni
mali zalishi, huwapeleka katika vikao mbalimbali vya kibiashara wanavyokutana
na wafanyabiashara wengine ili kuwazoeza namna kufanya biashara mbalimbali na hii ndio sababu ya matajiri huendelea kuwa matajiri.
Sasa naomba nikushirikishe jambo moja nalo ni Ili uweze kuwa
tajiri unatakiwa uwe unajiuliza swali hili JE NIFANYE NINI ILI NIWEZE
KUBADILISHA NA WATU KWA PESA ZAO?
Kwa sababu ulimwengu huu tunaoishi ni wa mbadilishano yaani
kuanzia unachotumia kuanzia asubuhi mpaka jioni umetumia pesa ndio maana
ukaweza kumudu kuvitumia kuanzia mswaki, dawa ya mswaki, ngo unazovaa, chai
unayokunywa na kitafunwa chake usafiri unaokupeleka kazini na kurejea nyumbani
vyote hivi umebadilishana kwa pesa. Kwa hiyo pesa zote ulizonazo sio zako kwa
sababu zinaenda kununua mahitaji yako ya siku nzima usijali Siku nyingine Mungu
akitujaalia nitakushirikisha namna ya kufanya pesa zako kuwa zako
Pia ili uweze kuwa tajiri lazima ujue maana ya mali na aina
za mali
Mali ni kitu chochote chenye thamani iwe kubwa au ndogo
ulichonacho kwa mfano simu, nyumba, gari, seti ya tv, radio,nguo za bei ghali
kama suti, kuwa na kiwanja, sasa mali hizi zinakupa faraja ya kihisia tu kwamba
nawe ni tajiri kwa kuwa unazo lakini ukweli ni kwamba kama hazikuiingizii
chochote wewe sio tajiri kwa sababu
huingizi chochote kutokana na mali hizo
Pia kuna Aina za mali nazo ni mali matumizi na mali zalishi ambapo mali
matumizi ni zile mali zinazotumia kipato chako kila siku mfano ukiwa na gari linahitaji mafuta ili liweze kutembea,
unatakiwa ulipie road licence, bima na ufanyie service kila mwezi lakini
halikuingizii chochote katika kipato chako cha siku ingawa inakurahisihia
shughuli zako na mali zalishi ni zile mali ambazo zinakuingizia pesa kila siku
mfano kuwa na nyumba ya kupangisha
wageni yaani guest house, kibanda cha kupigishia simu na au kuonesha
mpira wa miguu na filamu, bajai unayoikodisha kwa ajili ya usafiri na kadhalika
hizi ndio mali zalishi kwa sababu zinakuingizia kipato kila siku sasa hapa
katika mali zalishi pia ujue kasi yake ya kukuingizia kipato ni ipi mfano mwenye nyumba ya kupangisha
anapata pesa kwa mwezi kwa hiyo kasi yake ya kuingiza pesa ni ndogo
ukilinginisha mwenye nyumba anyefanya biashara ya kupangishia wageni kwa siku
yeye huingiza pesa kila siku na hivyo kasi yake ya kuingiza pesa ni kubwa
kuliko yule mwenye nyumba ya kupangisha anayesubiri mpaka mwezi uishe ndio
apate kipato chake.
Ukishafahamu mali, mali matumizi na mali zalishi utaweka
vipaumbele ni aina gani ya mali utanunua ili iweze kukukomboa toka katika lindi
la umaskini anza kujaribu kufikiria kuwa
na mali zalishi nyingi Zaidi kuliko mali matumizi wataalamu wa uchumi wanaamini kuwa ili uweze kufanikiwa kiuchumi unatakiwa uwe na mali zalishi zisizopungua saba ndio unaweza kukaa na kusema sasa unaelekea katika ulimwengu wa mafanikio.
Ukiamua kubadilika kifikra utakuwa ni mmoja wa watu
wataakaofanikiwa Zaidi kiuchumi na utapunguza kundi la watu maskini duniani na
kuingia katika kundi la matajiri na kurithisha vizazi vyako vyote kuwa matajiri
kwa kuwarithisha mbinu na maarifa ya jinsi ya kujikwamua kiuchumi wataalamu wa
sosholojia wanaitaa hii ni social mobility yaani ni jinsi ya kutoka jamii moja
kwenda jamii nyimngine mfano kutoka umaskini kwenda utajiri ni kazi ngumu sana
lakinii inawezekana jaribu utaona
ASANTE KWA KUSOMA MAKALA HII UKIWA NA SWALI, MAONI AU USHAURI
USISITE KUWASILIANA NAMI
NGOBOLE, Andrea Ashery.
0755780131
facebook.com/ Andrea Ngobole
facebook page, instergram na twiter ni princemediatz
Post a Comment