PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: FADHER NKWERA AONYA NA KUTAHADHARISHA SIASA KATIKA MADHABAHU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Padre Felician Nkwera Kiongozi wa Kikundi cha Sala cha Wanamaombi, Padre Felician Nkwera amesema nafasi ya Kanisa katika kuhakikisha mch...

Padre Felician Nkwera

Kiongozi wa Kikundi cha Sala cha Wanamaombi, Padre Felician Nkwera amesema nafasi ya Kanisa katika kuhakikisha mchakato wa kupata Katiba mpya unafanikiwa, ni kufunga na kumwomba Mwenyezi Mungu ili awapatie Watanzania Katiba wanayoitaka.

Alisema ushauri ambao Kanisa linatakiwa kuutoa kwa viongozi wa serikali na vyama vya kisiasa ni kufunga na kusali.

Padre Nkwera alikuwa akijibu maswali kuhusu nafasi ya Kanisa katika kuhakikisha Tanzania inapata Katiba itakayojibu kero za wananchi.

Alisema ni kosa kwa viongozi wa dini kutumia madhabahu yao kuisema serikali pamoja na vyama wa siasa, kinachotakiwa kufanyika ni kuwaita viongozi wa pande zote mbili zinazosigana ili kuzishauri namna ya kufikia mwafaka.

“Kanisa siyo wanasiasa, zamani kazi kubwa ya manabii ilikuwa kumuomba Mungu miongozo yake kwenye masuala mbali mbali.

Manabii walifunga na kumuomba Mungu awape majibu katika masuala ya vita, njaa au shida yoyote iliyolihusu taifa, walimuomba Mungu awasaidie kuwatatulia,” alifafanua.

Kwa sasa Tanzania iko katika mchakato wa kutunga Katiba mpya yenye lengo la kukidhi mahitaji ya wananchi wengi. Katika mchakato huo kumekuwa na mvutano ambao umesababisha mgawanyo wa makundi mawili ya Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) na Tanzania Kwanza.

Padre Nkwera alisema nchi itapata Katiba lakini siyo kwa kasi tunayoihitaji sisi kama binadamu. Tanzania ina wenyewe na wao ndio watakaoamua lini Tanzania iwe na Katiba mpya.

“Katiba itapatikana lakini siyo kwa spidi tunayoitaka, itapatikana hata katika kipindi cha awamu inayofuata,”
alisema.

Aliwataka Wanamaombi waombe ili Taifa lipate Katiba mpya inayofaa, kwani ni jukumu walilokabidhiwa kuombea mchakato huo ili nchi ipate Katiba mpya katika hali ya utulivu.

Alisema malumbano ya kwenye vyombo vya habari hayatatoa mshindi na badala yake malumbano hayo yataendelea kuivuruga Serikali na kusababisha kutokuelewana kuendelea.

“Jukumu la viongozi wa dini ni kuwashauri viongozi wa Serikali na wale wa vyama vya siasa ili wafikie mwafaka ambao utasaidia kupatikana kwa Katiba ambayo wananchi wanaitamani,” alisema.

Alipoulizwa iwapo Katiba haitapatikana Watanzania wafanye nini, Padre Nkwera alijibu kuwa zamani Waisraeli waling’ang’ania kuwa na mfalme wao kama yalivyo mataifa mengine, Mwenyezi Mungu akawaambia “Nikiwapatia mfalme atawafanya watumwa na atawalipisha kodi, hamtakuwa na amani”.

Waisraeli hawakumsikiliza na badala yake wakaendelea kung’ang’ania mfalme wao, Musa akamwambia Mwenyezi Mungu, “Waisraeli hawakupingi wewe bali wananipinga mimi, wapatie mfalme wao”. Mungu aliwapatia Saulo kuwa mfalme wao na toka siku hiyo walikumbuka maagizo ya Mungu.

Akizungumzia suala la upande upi Wanamaombi wasimamie kati ya kikundi kinachojiita UKAWA au Tanzania Kwanza, Padre Nkwera alisema Wanamaombi hawatakiwi kuwa na upande wowote kati ya hizo mbili, wanatakiwa kuwa neutral ndio maana wamepewa jukumu la kuombea mchakato.

Aidha alisema serikali tatu zitabomoa Muungano kwa sababu, serikali ya tatu haitakuwa na sehemu ya kupata mapato yake zaidi ya kutegemea nchi wahisani.

Alisema hatari ya kutegemea mapato kutoka kwa nchi wahisani ni pale nchi moja itakapogoma kutoa fedha kwa nchi ya tatu.

Alisema Tanzania ni nchi ya serikali mbili lakini uroho wa madaraka ndio unaosababisha watake serikali tatu.

Padre Nkwera alisema ili serikali mbili zifanye kazi, Zanzibar haina budi kufunga balozi zote ambazo imeingia nazo uhusiano, iondoe Katiba yake, iondoe bendera na hata wimbo wa Taifa, nchi iwe na bendera moja, wimbo mmoja wa Kaifa na Katiba moja.

Kwa kufanya hivyo Muungano utaendelea kudumishwa vizazi kwa vizazi.

Alitahadharisha kuwa serikali tatu siyo suluhisho la matatizo yaliyopo nchini bali ni kuongeza matatizo na hatimaye kuubomoa Muungano ambapo mwisho wake hautakuwa mzuri.

Katiba Pendekezwa itachapishwa upya; Mjumbe wa NCCR-Mageuzi alijumuishwa kimakosa
Posted by Krantz Mwantepele on 9:59:00 AM. - No comments

Uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba, umemuagiza Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, kupiga chapa upya Katiba Inayopendekezwa, baada ya kubaini makosa ya uchapaji, ikiwemo kuandikwa kwa makosa kwa mjumbe wa bunge hilo kupitia NCCR-Mageuzi Zanzibar, Haji Ambar Khamis.

Katika chapisho la Katiba Inayopendekezwa, mjumbe Khamis ameonekana kama vile alishiriki katika awamu ya pili ya Bunge Maalumu la Katiba, wakati hakushiriki.

Kosa hilo na mengine ya uchapaji, yamekuwa yakitumika kwa makusudi kupotosha umma kuwa Katiba Inayopendekezwa, ilipita katika mazingira ya kuchakachua kura za wajumbe, ili kuiondolea uhalali wake wakati wa kupiga kura ya maoni.

Moja ya jitihada hizo ni pamoja na hatua ya mjumbe Khamis, kuangua kilio
juzi mbele ya waandishi wa habari na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu, baada ya kukiri chini ya kiapo cha chama chake cha NCCR-Mageuzi, kuwa hakushiriki kuipitisha Katiba Inayopendekezwa.

Akizungumza na mwandishi jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Naibu Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Dk Thomas Kashililah, alisema jina la Khamis kuwepo katika orodha hiyo, ni moja kati ya makosa kadhaa yaliyobainika.

“Sisi tulibaini kasoro hiyo na mengine ya uchapaji siku ya kukabidhi Katiba hiyo Pendekezwa na kuelekeza Katiba hiyo ichapishwe upya baada ya kufanyiwa marekebisho,” alisema Dk Kashililah.

Alifafanua kuwa kuna vitabu vya aina mbili, kimoja kinachotumika kwa ajili ya kumbukumbu, ambacho kina majina ya wajumbe wote wa Bunge Maalumu la Katiba, wakiwemo wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wajumbe wengine ambao si wa Ukawa, lakini hawakushiriki kupiga kura.

Kitabu cha pili kwa mujibu Dk Kashililah, kimeorodhesha majina ya washiriki wa Bunge hilo katika awamu zote, ambacho wajumbe wa UKAWA na wengine ambao si wa kundi hilo hawapo kwa kuwa hawakushiriki mpaka mwisho.

“Baada ya kurekebisha (kile kitabu cha kumbukumbu) ili kupata kitabu kinachoeleza wajumbe waliopitisha Katiba Inayopendekezwa, jina hilo lilipita kimakosa wakati hakupiga kura, tunathibitisha hilo kosa kwa kuwa ni kweli hakuwepo kupitisha Katiba hiyo,” alisema.

Alifafanua kuwa katika orodha ya wapigakura, Mjumbe huyo wa NCCR-Mageuzi, alikuwa namba 63 lakini hakupigakura jambo ambalo haliathiri hata kidogo kura zilizopitisha Katiba Inayopendekezwa.

Pia Dk Kashililah alitoa ufafanuzi kuhusu wajumbe waliopiga kura kwa kusema jumla walikuwa 631, lakini baada ya mmoja kufariki walibaki 630 na kati yao, 411 walikuwa wa Tanzania Bara na 219 wa Zanzibar.

Alisema idadi hiyo ilipatikana baada ya mjumbe Salim Suleiman Ally kuondolewa Zanzibar na kuwekwa upande wa Tanzania Bara baada ya kuwekwa Zanzibar kimakosa.

Katika upande wa Zanzibar theluthi mbili ya kura zilizotakiwa kupitisha Katiba Inayopendekezwa, zilipaswa kuwa 146, hata hivyo Katiba hiyo kila ibara ilipitishwa kwa wastani wa kura 146 na 148.

Kwa upande wa Tanzania Bara, wajumbe 335 walipiga kura ambapo kila ibara ilipata wastani wa kura 331 mpaka 334, na hivyo kuzidi theluthi mbili iliyokuwa ikihitajika ya 274.

Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete, amewataka Watanzania kupuuza watu wachache wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya, na badala yake wajiandae kuipigia kura ya kuikubali wakati ukiwadia.

Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa nyakati tofauti juzi kwa wananchi mkoani Mwanza ambako yupo katika ziara ya kikazi ya siku tatu, kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.

“Watakuja watu kuwashawishi kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya, wasikilizeni lakini tumieni akili yenu, kama ile hadithi ya mbayuwayu. Jiandaeni tu kupiga kura na kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa kwa sababu hii ni Katiba nzuri sana,” alisema Rais Kikwete.

Alishangaa watu wanaodai kuwa Katiba Inayopendekezwa ni mbaya, akiuliza kuwa kama Katiba hiyo ni mbaya basi hiyo nzuri ikoje?

Aliisifu Katiba Inayopendekezwa kwa kujali makundi yote ndani ya jamii na kusisitiza kwamba kamwe haiwezi kuwa Katiba mbaya.

“Sijui Katiba nyingine duniani ambayo inajadili makundi yote ndani ya jamii kama hii Katiba Inayopendekezwa. Hakuna aliyeachwa – wavuvi wamo, wajane wamo, wafanyabiashara ndogo wamo, akinamama lishe wamo, wakulima wamo, wafungaji wamo….kila mtu yumo. Akinamama ndio usiseme kabisa wao wamepata hata asilimia 50 kwa 50 ndani ya Bunge,” alisema Rais Kikwete.

Aliongeza Rais Kikwete: ”Hivi katiba mbaya inakuwa kama inayopendekezwa na kama hii inayopendekezwa ni mbaya sasa hivi nzuri ikoje?” - See more at: http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com/2014/10/katiba-pendekezwa-itachapishwa-upya.html#.VDopxRbkQ8M

About Author

Advertisement

Post a Comment

Top