PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Warembo Wapanga Foleni Studio kwa Diamond Usiku wa Manane
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Wakati mzazi mwenza wa mkali wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa...
Wakati mzazi mwenza wa mkali wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa bize na malezi ya mtoto wao wa pili, Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’, habari zilizovuja kutoka kwenye studio za mkali huyo wa Ngoma ya Salome, WCB zilizopo Sinza- Mori, ni kwamba warembo wamekuwa wakipanga foleni nje ya studio hizo kumsubiri Diamond mpaka usiku wa manane.

Kwa mujibu wa taarifa zilizofika kwenye dawati la Gazeti la Risasi Jumamosi, warembo wa kila aina wamekuwa wakipigana vikumbo nje ya studio hiyo, kila mmoja akitaka kuonana na Simba, huku kila mmoja akikataa kuelewa waziwazi sababu ya kutaka kuonana na msanii huyo.

Taarifa zaidi zikazidi kueleza kwamba, kwa kawaida Diamond na kruu yake ya WCB hupendelea kuzama studio usiku kwa ajili ya kurekodi, hivyo wakati mwingine, warembo hao huonekana kwa wingi mpaka mishale ya usiku mnene.

Chanzo chetu kilizidi kutung’ata sikio kwamba inapotokea Diamond amemaliza kurekodi na anatoka, tayari kwa safari ya kurejea nyumbani kwake, Madale au kwa mama yake, Tandale, warembo hao huanza kumgombea, kila mmoja akitaka kupata nafasi ya kuzungumza naye.

Ikadaiwa kwamba, wakati mwingine kama wewe si mwenyeji wa mitaa hiyo, ukipita unaweza kudhani kuwa akina dada hao wanafanya biashara haramu ya kuuza miili yao kwani si kawaida kukuta warembo wakiwa wamejipanga nje, tena usiku wa manane.

“Unajua kama ukipita pale Wasafi usiku halafu ukawa ni mgeni unaweza ukadhani kuna danguro la akina dada wanaouza miili.
 "Lakini ukweli ni kwamba wale ni wanawake ambao wanakuwa wanamuwinda Diamond, akiingia au akitoka maana wanajua muda wake,” kilisema chanzo chetu na kuongeza kuwa wakati wengine wakimgombea Diamond, wengine husambaa kwa memba wengine wa kundi hilo, wakiwemo Rich Mavoko, Rayvanny, Harmonize na mastaa wengine.diamond-8

Baada ya kupata ubuyu huo, kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM), kama kawaida yake, kilitinga eneo la tukio, WCB ili kudodosa ukweli wa taarifa hizo ambapo baada ya kufika kilikutana na mlinzi aliyekuwa zamu katika studio hizo (picha tunazo).

Bila kujitambulisha kuwa ni waandishi waliokuwa hapo kwa kazi maalum, OFM walianza shughuli yao ya upelelezi kwa kupiga stori na mlinzi huyo ambaye alijikuta akiingia kwenye kumi na nane na kusimulia ishu nzima.

“Ni kweli warembo huwa wanajipanga hapo usiku inakuwa ni ishu kabisa hata rais (Diamond) anapokuwepo. Tukiwafukuza huwa wanasema wanamsubiria Diamond, si unajua tena bwana mkubwa anafanya kazi zake za studio zaidi usiku?
“Sasa akishamaliza kufanya yake, akitoka ndipo anapokutana nao kila mmoja akitaka  aondoke naye, wengine wanasema huwa wanasikia ni sukari ya warembo hivyo nao wanataka kuona kama hiyo sukari ni sukari ya aina gani,” alisema mlinzi huyo.

Mlinzi huyo aliendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi kuwa, warembo hao huwa wanakasirika wanapomuona akitoka na mrembo (anataja jina la staa wa kike ambaye aliwahi kudaiwa kutoka na Diamond kimapenzi) ambaye ilielezwa kwamba hupenda kuja kumchukua jamaa huyo na kusepa naye.

“Si hao tu wanaojipanga, wapo hata wale mademu ambao vyombo vya habari vimekuwa vikiwaandika mara kwa mara kuwa wanatoka naye kimapenzi, huwa wanamfuata hapa na kuondoka naye,” alisema mlinzi huyo akirekodiwa sauti.

Baada ya makachero wa OFM kumalizana na mlinzi huyo, walianza kazi maalum ya kumtafuta Diamond ambaye hakuwemo studio lakini hadi usiku mnene hakutokea. Kama hiyo haitoshi, siku iliyofuata, makachero wetu walitinga tena kwenye studio hizo majira ya mchana na kupiga kambi kumvizia lakini hakuonekana, kwa sababu alikuwa nchini Gabon kwenye uzinduzi wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).

GPL

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top