NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.
Kituo
cha kukuza mchezo wa mpira wa Miguu kutoka nchini Kenya cha Trans Nzoia
Youth Sports Association ( TYSA) kimetua Mkoania Arusha na kusaidia
baadhi ya watoto ili kuwahamasisha katika mchezo wa Huo.
Ofisa
wa kukuza michezo katika kituo hicho Francis Ojilo alisema kuwa
wameamua kusaidia watoto ili kuhakikisha vijana wanakua na elimu ya
michezo pamoja na nidhamu hivyo jamii nzima itanufaika na program ambayo
wanaifanya.
“Tupo
na watoto kutoka sehemu mbalimbali hapa Mkoani Arusha na tunawafundisha
mambo tofauti tofauti kuhusu michezo na hata ya kijamii, Mfano
tunamjenga mtoto kutambua kipaji chake na kuwasaidia katika nidhamu ya
michezo” alisema Ojilo.
“Hatumfundishi
mtoto jinsi ya kufunga tu, ila tunamfundisha jinsi ya kukaba, kutoa
pasi na kuisaidia timu inapozidiwa na hata inapohitaji kulinda ushindi
ambao wameshaupata”
Hata
hivyo Ojilo alisema kuwa michezo husaidia kwa kiwango kikubwa kwa mtoto
kuwa na akili nyingi hata kufanya vizuri akiwa darasani.
“Wazazi
tunashirikiana nao vizuri kwa sababu huwa tunafanya mikutano mbalimbali
na wazazi, na walimu kutoka shule ambazo watoto wanasoma hivyo kila mtu
ananafasi ya kuhakikisha mwanae anafanikiwa” Alisema Ojilo.
TYSA wapo jijini hapa katika ushiriki wa tamasha la Zinduka lilianza kufanyika juzi alihamisi na likitarajia kumalizika leo jumamosi, tamasha la Zinduka linashirikisha Nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.
Ojilo
aliongeza kuwa tatizo kubwa linalowakabili wanamichezo katika jumuiya
ya Afrika Mashariki ni kuwa na uongozi usiojua majukumu yao ipasavyo
hasa ya kuendelea michezo na kutokuwa na ushirikiano mzuri na wadau
mbali mbali wa michezo.
Post a Comment