PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: AFC, MADNI FC MZIGONI KANDA YA ZIWA.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA; YOHANA CHALLE. ARUSHA. Timu ya AFC ya jijini hapa na timu ya Madini Fc yenye makazi yake mkoani Manyara leo jumamosi  wanaingia...
NA; YOHANA CHALLE.
ARUSHA.

Timu ya AFC ya jijini hapa na timu ya Madini Fc yenye makazi yake mkoani Manyaraleo jumamosi wanaingia kibaruani Kanda ya Ziwa katika mwendelezo wa ligi daraja la pili ngazi ya Taifa (SDL).

AFC itakuwa ikikaribishwa na timu ya Alliance Fc kutoka mkoani Mwanza, wakati Madini Fc watakuwa wakicheza na JKT Rwankome ya Mkoani Mara.

Katika michezo ya ufunguzi ya SDL Timu zote ziliambulia vichapo,AFC wakiwa ugenini ilifungwa na timu ya Pamba kwa mabao 3-0 wakati Madini Fc nayo iliambulia kichapo cha Mabao 2-0 dhidi ya timu ya Alliance FC.

Hata hivyo AFC imekuwa na matokeo mabaya katika michezo yake ya hivi karibuni kwani ilipoteza tena katika mchezo na Madini FC kwenye mwendelezo wa mashindano ya Shirikisho (FA) Kwa mabao 2-0.

Hata hivyo katibu msaidizi wa AFC Charles Mwaimu Alisema kuwa tayari kikosi hicho kimefanyiwa marekebisho ya kutosha na wanauhakika wa kushinda mchezo wa Leo (jumamosi) dhidi ya Alliance Fc.

Mara ya kutoka Kanda ya ziwa timu zote zitakuwa nyumbani, AFC wakiikaribishaJKT Rwankome katika uwanja wao wa Sheikh Amri Abeidi huku Madin Fc wakiikaribisha Bulyanhulu FC kutoka Mkoani Shinyanga.
 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top