Mchezaji wa Vishale
wa timu ya
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Zahra Kitala akiwa kwenye moja ya mchezo huo katika mashindano ya
SHIMMUTA yanayoendelea jijini Arusha. Picha
na Yohana Challe
|
NA; YOHANA
CHALLE.
ARUSHA.
Mashindano
ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) yanayojumuisha
jumla ya michezo 12 yanayoendelea jijini hapa yameanza kutoa mabingwa kwa
baadhi ya michezo ambapo imeshuhudiwa timu Ya NEMC ikifanikiwa kuibuka mabingwa
katika mchezo wa Vishale (Darts) kwa upande wa wanawake.
NEMC walifanikiwa
kutangazwa washindi baada ya kuwatoa wapinzani wao katika mchezo wa
fainali , timu ya chuo kikuu Ardhi ambao waliambulia nafasi ya pili huku nafasi
ya tatu ikiwaendea timu ya Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu.
Kwa upande
wa mchezo wa Pool Table kwa wanaume Mshindi wa kwanza
iliwaendea shirika la viwango nchini TBS, nafasi ya pili kushikiliwa
na chuo cha ufundi Arusha (ATC) Huku Nafasi ya tatu ikiwaendea Shirika la
hifadhi la mazingira Taifa (NEMC).
Katika michezo
mingine ikiwemo riadha inatarajiwa kufanyika siku ya ijumaa ambapo washiriki
wataweza kukimbia mita 100,200 na 400,na Michuano hiyo inatarajia kufika tamati
Novemba 30 .
Aidha mbali
na michezo hiyo ,pia kumekuwa na taarifa ya baadhi ya timu shiriki kukata
rufaa kwa kamati tendaji ya SHIMMUTA zikipinga baadhi ya timu kuhusisha
wachezaji ambao ni mammluki.
“Kweli sisi kama
kamati ya SHIMUTA tumepokea malalamiko kutoka timu ya shirika la maendeleao ya
Petroli nchini (TPDC ) Katika mchezo wa mpira wa miguu, ambayo imekata
rufaa dhidi ya timu ya bodi ya mikopo ya Elimu ya juu wakilalamikia
kuchezesha wachezaji 6 ambao sio wahusika yaani Mamluki” alisema katibu
wa SHIMMUTA Award Safari.
Alieleza
kuwa mara baada ya Uchunguzi kukamilika dhidi ya malalamiko hayo
yaliyotolewa na timu ya TPDFC kamati ya Nidhamu itatoa majibu juu ya tuhuma
zilizotolewa ambapo sheria za mashindano zitachukua nafasi yake.
Michezo mingine
ikiwemo Mpira wa Miguu,Mpira wa pete,Mpira wa kikapu itaendelea leo Ijumaa katika viwanja vya General
Tyre katika hatua za robo fainali.
Post a Comment