Mashindano
ya riadha yajulikanayo kama Mount Meru Marathon yanatarajia kufanyika oktoba 4
mwaka huu jijini hapa kwa kushirikisha wanariadha kutoka sehemu mbalimbali
ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumza
na gazeti hili Mratibu wa mashindano hayo Gidamis Shahanga alisema kuwa
mashindano hayo yataanzia mnara wa saa na kwenda uwanja wa ndege na
kuhitimishwa katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
“mashindano
haya chimbuko lake ni mkoani hapa na mara ya mwisho kufanyika ilikuwa mwaka 20000
kipindi hicho yakiwa yanaitwa , Mount Meru International Marathon, hivyo
tulisimama kutokana na mambo kuto kuwa mazuri hasa kwa upande wa fedha” alisema
Shahanga.
Shahanga
ambaye pia ni katibu wa Chama cha Riadha mkoani hapa, aliongeza kuwa mashindano
hayo yamegawanyika katika makundi mbalimbali, kutakuwa na mbio za 21km ambapo
mshindi atajinyakulia kiasi cha sh 200,000.
Pia kutakuwa
na mbio za 5km ambazo hakuweza kuweka bayana zawadi ya mshindi huku akisisitiza
kuwa 5km zitakuwa kwa watu maalumu kama vile wazee.
Mashindano
hayo ni ya wazi ambapo mtu yoyote anaruhushiwa kushiriki hata kama sio
mtanzania, ilimradi amefuata taratibu na kanuni zote zitakazowekwa ikiwa pamoja
na kujiandikisha kwa muda muafaka.
Mashindano
hayo yanaandaliwa na kampuni ya Mambo leo Digital Centre kwa kushirikiana na
chama cha riadha mkoa wa Arusha, huku wadhamini wakuu wakiwa ni SBL.
Usajili kwa
washiriki utaanza septemba 20 na kumalizika Oktoba 3 jioni katika uwanja wa
Sheikh Amri Abeid, na Arusha Hoteri ambao pia ni wadhamini.
Post a Comment