Wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Wakili Msomi Awadh Ali amesema kuwa
uchaguzi wa marudio wa Zanzibar haupo kisheria. Wakili Awadh,akihojiwa
na ITV,amesema kuwa Katiba na Sheria ya Uchaguzi wa Zanzibar haitambui
uchaguzi wa marudio.
Wakili Awadh amesema kinachofanywa na ZEC ni kuwashurutisha wanasiasa na
wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio hapo Machi 20. Wakili
Awadh amesema kuwa washindi wa uchaguzi wa mwaka jana walishapewa vyeti
vya ushindi na hivyo hawawezi kupokwa vyeti vyao.
Kuhusu pendekezo la kukimbilia mahakamani kupinga uchaguzi wa
marudio,Wakili Awadh amesema kuwa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja
na Katiba haziruhusu kupingwa au kuchunguza ZEC kimahakama.
Post a Comment