Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Mkoma, akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu akihutubia katika uzinduzi huo.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy,
akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick
Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu Lucy Mshomi wa Shule ya
Wasichana ya Kifungiro kutokana na mchango mkubwa kwa wanafunzi wao.
Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick
Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu Josephine Mashare wa Shule
ya Wasichana ya ST' Marys ya Mazinde Juu kutokana na mchango mkubwa kwa
wanafunzi wao.Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus
Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa
Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi mwanafunzi mshindi wa
kwanza kitaifa wa kuandika barua, Glory Mduma kutoka Shule ya Sekondari
ya ST, Marys Mazinde Juu mkoani Tanga. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick
Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mshindi wa tatu wa shindano hilo,
Khadija Rashid wa Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu. Kulia
ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi
mwanafunzi mshindi wa pili kitaifa wa kuandika barua , Ndehovye Nyindo wa Shule ya Wasichana ya Lufungiro iliyopo mkoani humo.
Wanafunzi
ambao ni washindi wa shindano la kuandika barua wakiwa katika picha ya
pamoja na zawadi zao walizokabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu kwa niaba
ya Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa katika hafla ya
ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Posta Duniani 2014 yaliyofanyika
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dar es Salaam leo. Kutoka
kushoto ni mshindi wa kwanza kitaifa wa shindano hilo, Glory Mduma
kutoka Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi
wa pili, Ndehovye Nyindo wa Shule ya Lufingiro mkoani humo, na Mshindi
wa tatu, Khadija Rashid wa Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde
Juu.
Wanafunzi, Wazazi na wageni waalikwa wakiwa
kwenye hafla hiyo.

WANAFUNZI
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St Mary's ya Mazinde Juu iliyopo
mkoani Tanga wameibuka vinara wa shindano la uandishi wa barua
lililoshirikisha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini katika kuadhimisha
siku ya posta duniani.
Shindano hilo la uandishi wa barua limeratibiwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa posta duniani.
Akizungumza
Dar es saalam leo katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya
posta duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Posta nchini, Deus Mdeme alitoa
pongezi kwa washindi hao na walimu wao kwa kufanikiwa kuibuka videdea
ambapo mshindi wa kwanza ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
barua ya kimataifa yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Uswisi.
"Madhumuni ya shindano hili ni kuwajengea uwezo vijana ambao hawajazidi miaka 15'' alisema Mdeme.
Katika
Shindano hilo la uandishi wa barua jumla ya washindi kumi walipatikana,
huku St Mary Mazinde juu wakiibuka videdea kwa kutoa washindi wawili
huku mshindi wa pili akitoka Shule ya Sekondari ya Lufingilo mkoani humo
ambapo walikabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali.
Aidha
katika kuadhimisha siku hiyo ya posta duniani, yenye kauli mbiu isemayo
posta inachukua nafasi yake katika mageuzi ya sekta ya mawasiliano
imeadhimishwa kwa kuelezea malengo na changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya Posta Tanzania.
Wakati
huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Profesa Patrick Makungu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa
Makame Mbarawa, alielezea mafanikio na changamoto mbalimbali
zinazoikabili Sekta ya Posta Tanzania katika kufanikisha malengo yake.
Vilevile
alitumia nafasi hiyo kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kushiriki katika
shindano hilo linaloandaliwa na umoja wa posta duniani na kuwataka
wadau wa posta nchini kushirikiana na shirika hilo ili likue na kutoa
huduma kwa jamii baada ya kubadilisha ufumo wa utoaji huduza zake kwa
kutumia zaida Tehama.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.