Hii ndiyo picha ya askari hao iliyozagaa kwenye mitandao ya kijamii wakila ujana na sare za kazi.
JESHI la polisi mkoani Kagera,
limewafuta kazi askari watatu kwa kosa la kupiga picha zilizo kinyume na
maadili na kuzisambaza mitandaoni.
picha hiyo hapo juu kuanzia jana ilikuwa ikisambaa kwa kasi katika mitandao mbalimbali ya kijamii kama facebook na WhatsApp ambapo ilikuwa na vichwa mbalimbali vinavyoelezea uovu huo uliofanywa na askari hao.
|
Kamanda a Polisi Mkoani Kagera Henry
Mwaibambe amewataja askari hao kuwa ni
PC ASUMA MPAJI MWASUMBI mwenye
namba F. 7788,
PC FADHIL LINGA mwenye namba G.2122
na WP VERONICA NAZAREMO
MDEME
wote walikuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya
Misenyi.
Mwaibambe, amemtaja PC FADHIL kuwa ndiye
aliyepiga picha hiyo na kuisambaza mitandaoni kinyume cha sheria na
kuisambaza mitandaoni.
Post a Comment