mwandishi wetu, Babati.
Wakala
wa barabara(TANROADS) mkoa wa Manyara, imetangaza mkakati wa kuongeza
alama za barabarani katika eneo la mapito ya wanyama kutoka minjingu
hadi Mdori.
Akizungumza
na wanahabari,Meneja wa TANROADS, mkoa wa Manyara Mhandisi, Bashiri
Rwesingisa, alisema wameamua kuongeza alama za barabarani katika eneo
hilo ili kupunguza ajali za binaadamu na vifo vya wanyamapori.
"lile
eneo pale hatuwezi kuweka matuta ila tutaongeza alama za wanyama kwani
ni ukweli kuwa ajali zinatokana na wanyama kuvuka katika eneo hilo
ambalo lina msitu"alisema
Alisema
miongoni mwa alama ambazo zitaongezwa ni michoro na mabango ambavyo
vitaonesha eneo hilo lina idadi kubwa ya wanyamapori hivyo, dereva
achukuwe tahadhari.
Rwesingisa
alisema TANROADs ipo tayari kushirikiana na wadau wa usalama barabarani
na wadau wa utalii, ili kuhakikisha ajali za magari na wanyama
zinapungua katika eneo hilo lenye kilomita 13.
Awali
Meneja wa kampuni ya Chem chem,Charles Silivester na Mwenyekiti wa
jumuiya ya uhifadhi wanyamapori ya burunge(WMA),Ismail Ramadhani
walishauri eneo hilo kuwekwa matuta.
Silivester
alisema katika eneo hilo, kwa wiki moja wanyama wasiopungua wanne
ugonjwa hasa kutokana na mwendokasi wa madereva licha ya kuwepo alama za
wanyama.
"sisi
baada kuona ajali zinaongezeka na hii ya juzi ya waziri tuliomba matuta
na chemchem tupo tayari kushirikiana na TANROADS kupunguza hili
tatizo"alisema
Kwa
upande wake, Ramadhani alisema, jumuiya yao inasikitishwa na matukio ya
ajali katika eneo hilo na wanaamini linachangiwa na vitu vingi, ikiwepo
uvamizi wa watu katika maeneo ya mapito ya wanyama.
"tunataka
serikali ichukuwe hatua kulinda haya mapito sisi kama WMA tunafanya
kazi kubwa kulinda wanyama na sasa wameongezeka lakini uvamizi wa
shughuli za binaadamu umekuwa mkubwa"alisema
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla Augost 4, alipata ajali
katika eneo hilo, wakati gari alilokuwa amepanda kumkwepa Twiga na
katika ajali hiyo, afisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba alifariki na
wengine wawili kujeruhiwa.
Post a Comment