Baadhi ya wakurugenzi na viongozi wa Friedkin Conservation Fund wakiwa katika maonesho ya nanenane mwaka huu mkoani Simiyu |
Mwandishi wetu, Bariadi.
Zaidi ya Taasisi 30 ambazo zilichangia kufanikisha maonesho ya wakulima
na wafugaji Nane nane kitaifa mkoani Simiyu, zimepewa zawadi na
kupongezwa na kamati ya maandalizi ya maonesho hayo.
Katibu
tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sigini alisema maonesho ya wakulima na
wafugaji, nane nane mwaka 218 yamekuwa na mapinduzi makubwa kutokana na
ushiriki wa taasisi nyingi lakini pia uchangiaji wa maonesho hayo ambao
ulifanywa na wadau mbali mbali.
Sagini
alitaja baadhi ya taasisi ambazo zimechangia maonesho hayo kufana ni
Benki ya NBC, Taasisi ya uhifadhi a Friedkin Conservation Fund,Vituo vya
luninga vya TBC na Clouds,Suma JKT, NMB bank,taasisi mbali mbali za
umma ikiwepo halmashauri zote za mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na
mashirika binafsi.
Wakizungumza
kuhusiana na maadhimisho ya Nane nane, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthon
Mtaka, Mkuu wa mkoa wa Shinyaga, Zainab Telack na Mkuu wa mkoa wa Mara,
Adam Malima, walieleza maonesho ya mwaka huu, yamekuwa na mabadiliko
makubwa ambayo yanalenga mapinduzi ya kilimo na ufugaji katika kuelekea
Tanzania ya Viwanda.
Mtaka
alisema wameridhishwa na ushiriki wa wananchi wengi lakini pia aina ya
vipando, zana za kilimo na ufugaji na huduma mbali mbali, ikiwepo
kuvutia watalii, zilivyooneshwa katika maonesho hayo.
"viwanja
vya Nyakabindi havitakufa baada ya maonesho, tutahakikisha vinaendelea
kutumika na makundi mbali mbali katika kulima kilimo cha kisasa lakini
pia kutumika kama shamba darasa la kilimo na ufugaji wa kisasa"alisema
Alisema
katika maonesho ya mwakani, watajipanga kuwa ya kimataifa zaidi kwa
kualika taasisi nyingi za kimataifa sambamba na nchi jirani.
Baadhi
ya wakurugenzi wa taasisi zilizotunukiwa vyeti maalum, ikiwepo taasisi
ya Friedkin,walisema wameshiriki maonesho hayo, ili kuonesha umuhimu
wake, katika kufikia lengo la Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya
viwanda.
Mkurugenzi wa
Friedkin Conservation Fund(FCF) Abdurkadir Mohamed, alisema taasisi yao
ya utalii na uhifadhi, ilishiriki ili kuonesha mahusiano ya Utalii
katika Kilimo na ufugaji nchini.
"FCF
mdau wa maonesho kwani tunafanyakazi katika vijiji vya wakulima na
wafugaji, hivyo tunategemea malighafi kutoka kwao lakini pia
tunashirikiana katika uhifadhi wamazingira ili kupata mvua lakini pia
tunashirikiana katika vita dhidi ya ujangili ili wanyama wetu waendelee
kuwepo"alisema.
Post a Comment