Meneja Chemchem, Kanali mstaafu Leonard Werema, akizungumza na wakazi mbalimbali waliojitokeza katika ufunguzi wa mashindano hayo |
Mkuu wa wilaya ya Babati,Elizabethi Kitundu akionesha na kufurahia zawadi aliyokabidhiwa na kikundi cha akina mama wa kibarbaigi mara baada ya kutoa burudani kwa wageni waalikwa |
Mkurugenzi mkuu wa chemchem akifurahia ngoma na kikundi cha akina mama wa kikoi walipokuwa wakitoa burudani katika ufunguzi wa mashindano hayo |
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Augustine Senga akikagua kikosi cha mpira wa miguu cha super boys mara baada ya kuzindua mashindano ya chemchem cup yanayotimua vumbi mkoani Manyara. |
NA: ANDREA NGOBOLE, BABATI
Vijana
wilayani Babati mkoa wa Manyara, wametakiwa kushiriki katika vita dhidi
ya ujangili na uhifadhi wa Mazingira ili waendelee kunufaika mapato
yatokanayo ya sekta ya Utalii.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Manyara, Augustine Senga, alitoa wito huo jana katika
tamasha la kupiga vita Ujangili na uhifadhi wa Mazingira, lililoandaliwa
na Taasisi cha Chemchem wilayani Babati mkoa wa Manyara.
Kamanda
Senga alisema, ujangili sio tu, unapoteza rasilimali za nchi bali ni
makosa ya jinai kwani tayari serikali imepiga marufuku uwindaji haramu.
"sisi
sote hasa vijana tujuwe ni jukumu letu kupiga vita ujangili,kutunza
mazingira na kuacha tabia ya kuvamia katika maeneo yaliyohifadhiwa na
tukifanikiwa tutaendelea kupata faida kutoka sekta ya utalii"alisema
Hata
hivyo, Kamanda Senga alieleza uwepo wa tamasha hilo kumesaidia kuwepo
wa amani na utulivu kwa wananchi wa eneo hilo ambao wameunda jumuiya ya
uhifadhi ya wanyapori ya jamii(WMA) ya burunge tofauti na ilivyokuwa
miaka ya nyuma.
Awali
Meneja Chemchem, Kanali mstaafu Leonard Werema, alisema taasisi yao
ambayo inaendelesha hoteli za kitalii za chemchema na kitalu cha
uwindaji, katika eneo la tarafa ya Mbugwe,imeona itumie tamasha kutoa
elimu juu ya kupiga vita ujangili na uhifadhi wa mazingira.
"tunaamini
kupitia tamasha kama hili, watoto wadogo,wanafunzi, vijana na watu
wazima watapa elimu ya uhifadhi na kujua athari za ujangili"alisema
Alisema
taasisi hiyo tangu mwaka 2014 imekuwa ikiandaa tamasha hilo kwa
kukusanya vijana,wanafunzi na vikundi mbali mbali vya watu wazima, ili
kupata elimu ya uhifadhi.
Akizungumza
katika tamasha hilo, Mkuu wa wilaya ya Babati,Elizabethi Kitundu
alisema serikali inaunga mkono jitihada za uhifadhi na kupiga vita
ujangili ambazo zinaendelea wilayni Babati.
"leo
ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, nimejifuza mengi nawapongeza
Chemchem kwa kazi ya kutoa elimu ya kupambana na ujangili na kutunza
mazingira na serikali tutaendelea kutoa ushirikiano"alisema.
Tamasha
hilo, lilijumuisha ngoma za asili za kiberbeig, kimasai, kimbugwe na
michezo ikiwepo soka na mpira wa pite ambapo zaidi ya milioni 20
zinatarajiwa kutumika.
Post a Comment