Mgeni rasmi na baadhi ya viongozi wakikagua timu |
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa ligu hiyo |
Mashabiki mbalimbali waliojitokeza kushuhudia ligi hiyo |
akina mama wa upendo group wakitoa burudani |
Kikundi cha akina mama wa kibarbaigi wakitoa burudani katika mashindano hayo |
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elexander Mnyeti juzi, amezindua ligi ya
Chemchem ,inayoshirikisha timu 20, yenye lengo la kupiga vita ujangili
ambayo itagharimu zaidi ya sh 35 milioni.
Akizungumza
katika uzinduzi huo katika viwanja vya mdori, wilayani Babati, Mnyeti
ambaye aliwakilishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Augustine
Senga alitaka timu zitakazoshiriki kucheza kwa nidhamu ili kufikia
malengo ya ligi hiyo.
Mnyeti
alisema,ligi hiyo pia inapaswa kutumika katika kuibua vipaji kwa
wachezaji chipukizi ili kuweza kusajiliwa katika timu za ligi kuu.
"najua
hapa kuna vipaji hivyo michezo hii ni fursa ya kujulikana zaidi na
hivyo kuwa sehemu ya kutoa ajira kwa vijana na kujenga afya"alisema
Katibu
wa mashindano hayo,John Bura alisema jumla ya timu 20 za soka
zinatarajia kushiriki michuano hiyo na kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa
kwanza hadi wa nne.
"pia kutakuwa na ligi ya wanawake ambayo itashirikisha timu tatu na washindi watapewa zawadi"alisema
Alisema
katika michuano hiyo, mchezaji bora,mfungaji bora na timu yenye
nidhamu, watapata zawadi na hivyo, akawataka kucheza soka la kuvutia.
Awali
Meneja wa Chemchem ambao ni wadhamini wa ligi hiyo, Kanali
mstaafu,Leonard Werema alisema, taasisi hiyo, inayofanya shughuli za
Utalii katika eneo hilo la hifadhi ya jamii ya Wanyamapori(WMA) ya
burunge, inataka ligi hiyo, kusaidia kutoa elimu ya kupiga vita ujangili
na uhifadhi.
Werema
alisema Chemchem imegharamia zaidi ya sh 35 milioni katika michuano
hiyo, ikiwepo kuandaa uwanja na majengo kadhaa,zawadi, imetoa vifaa vya
michezo kwa timu zote 23 na gharama nyingi za waamuzi na waratibu wa
michuano hiyo chama cha soka wilaya ya Babati.
Katika
mchezo wa ufunguzi, mabingwa watetezi, Mdori FC walipata ushindi wa
magori 3-2 dhidi ya timu ya City Boys katika mchezo mkali uliochezwa
kiwanja cha mdori.
Post a Comment