Dr. Edward Kohi wa kituo cha utafiti wa wanyama pori TAWIRI akiwana Dr.Robert Fyumagwa wa TAWIRI wakimfunga kifaa cha mawasiliano tembo katika hifadhi ya Taifa Mikumi |
Mwandishi wetu,Mikumi
Taasisi
ya uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) imejitolea kufadhili
mradi wa kufungwa vifaa vya kufatilia mienendo yaTembo katika eneo la
Ikolojia ya Selous hadi hifadhi ya Taifa ya Mikumi mradi utakao gharimu
zaidi ya sh 1bilioni.
Akizungumzia
zoezi hilo.Mtafiti kiongozi wa TAWIRI, Dk.Edward Kohi alisema,mpango
huo utasaidia mapambano dhidi ya ujangili,kudhibiti Tembo kuvamia
mashamba na kujua mienendo yao.
Dk
Kohi alisema, mpango huo utakuwa wa miaka mitano na tayari tembo watano
wamefungwa vifaa hivyo vya mawasiliano katika eneo la hifadhi ya Taifa
ya Mikumi na awamu ya kwanza Tembo 13 watafungwa vifaa hivyo na katika
mradi wote tembo 60 watafungwa.
"tembo
ambao watafungwa collar ni viongozi wa makundi na baada ya kufungwa
watakuwa wanaonekana na wahifadhi kupitia mfumo wa mawasiliano ambao
umewekwa kila wanapokuwa" alisema
Akizindua
mpango huo,kwa niaba ya Mkurugenzi wa Wanyamapori, wizara ya Maliasili
na Utalii,Afisa wanyamapori mkuu,Silivernus Ukudo alisema mpango huo una
manufaa makubwa katika uhifadhi.
Ukudo
alisema, katika eneo la ikolojia ya Selous - Mikumi ndiko kuna tembo
wengi zaidi nchini ambao wanaokadiriwa kufikia 15,000.
Alisema
serikali inashukuru msaada uliotolewa na mashirika ya uhifadhi Friedkin
Conservation Fund na frankfurt zoological society na WWF kwa msaada
waliotoa kusaidia mpango huu.
Meneja
mawasiliano wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund,Clarence Msafiri
alisema, taasisi hiyo imejitolea kusaidia zoezi hilo kwani ni muhimu kwa
taifa.
Alisema FCF
ambayo kampuni zake kadha zimewekeza maeneo ya hifadhi nchini,inatambua
kama Tembo wakilindwa Wanyamapori wengine watakuwa salama.
"Katika zoezi hili muhimu tumetoa helkopta na misaada mingine ili kuwezesha Tembo kufungwa vifaa hivi vya mawasiliano" alisema
Mhifadhi
Mkuu wa hifadhi ya Mikumi,Godwell Ole Meng'ataki alisema zoezi la
kufungwa collar za mawasiliano litasaidia kupunguza migogoro ya uvamizi
katika mashamba ya vijiji 19 vinavyozunguka hifadhi ya Mikumi.
"Pia
tutaweza kufatilia maeneo ya mapito ya wanyama kutoka Mikumi hadi
maeneo ya Wami mbiki na hifadhi za kusini hadi nchi jirani ya Msumbuji"
alisema
Post a Comment