Nchi yoyote
haiwezi kuendelea pasipokuwepo na usalama madhubuti kwa taifa lake, maana
kuwepo kwa usalama kutawafanya wananchi kuishi kwa Amani na kujiamini pasipokuwa
na wasiwasi wowote wa vitendo vitakavyo vunja Amani.
Taifa
lenye Amani ya usalama mzuri halitegemei Jeshi ili kuleta Amani, wala
halitegemei mtu Fulani, au kiongozi Fulani akiwa madarakani au akiingia
madarakani basi ataweza kuleta usalama kwa taifa, laah hasha! Bali RAIA wa
taifa lenyewe ndilo wenyewajibu wa kulinda nchi yao.
Asilimia
kubwa ya usalama wa taifa inabebwa na RAIA kwa sababu wao ndio miongoni mwa
jamii na ndio wengi kuliko hata dola, na ndio wenye nguvu kuliko hata jeshi
bali jeshi ni sehemu tu ya kusimamia usalama wa Taifa.
RAIA
mwema kwa taifa lake hapendi kuona amani ya taifa lake inavulugwa na mtu,watu
au kikundi kwa manufaa yao binafsi hasara ikawa kwa taifa zima.
RAIA
mwema hapendi kuwa mkimbizi ndani ya taifa lake, kwani ni aibu kubwa kuomba
AMANI ukiwa katika taifa lako , ni fedhea kuomba sehemu ya kujihifadhi ukiwa
ndani ya nchi yako, ni vibya kuwa mtumwa ukiwa ndani ya nchi yako.
Lakini
hayo yote yanawezekana kutokea endapo mimi na wewe tusipo ilinda tunu ya AMANI
tuliyopewa na mwenzezi Mungu kwa muda mrefu, japo wahenga walisema kujenga ni
vigumu bali kubomoa ni rahisi.
Ndugu
zangu watanzania AMANI hii tunayojivunia kumbuka waliyoijenga wengi wamefariki na
ni katika harakati za kuijenga AMANI hii wengi walipoteza maisha, hivyo
tukumbuke kuwa tukiibomoa basi tuwe tayari kupoteza watu kwa ajili ya kuijenga
Upya AMANI hii.
Ukiangalia
siasa inavyoendelea katika nchi yetu utakuwa na jibu tosha juu ya AMANI ya
taifa hili, kuwa kiongozi ni haki ya kila mtu, kupiga kura ni haki ya kila mtu,
kumchagua kiongozi ni haki ya kila mtu. Lakini kumbuka haki haiji bila
kuwajibika.
Katika
katiba ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 sura kwanza sehemu ya
tatu, kifungu cha 17 (1) kinasema “kila raia wa jamuhuri ya Muungano anayo haki
ya kwenda kokote katika Jamuhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu
yoyote,kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au
kufukuzwa kutoka katika Jmuhuri ya Muungano”
Mtanzania
mwenzangu hayo yote yanaweza kuwa ndoto endapo hatutashiriki kikamilifu katika
ulinzi wa Taifa hili taijiri kwa AMANI.
Nchi
kuwa na AMANI au vita haitaji kuangalia kabira, elimu, wala Dini Fulani, maana
hali ikiwa mbaya kila mmoja ataona uchungu wake na kusahau hata kama una nyumba
nzuri, gari zuri au una pesa nyingi maana wote tutalala porini.
Ukiangalia
katika katiba ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 sura ya sita
sehemu ya kwanza, kifungu cha 130 (1) kupitia tume ya haki za Binadamu na
utawala bora itekeleze yafuatayo:
Mambo
mengi hufanywa na tume hiyo kwa ajili ya usalama na haki kwa wananchi wake, ila
wananchi tuna wajibu mkubwa kuliko hata tume katika kulinda usalama wa taifa
letu.
Hata
hivyo viongozi wetu wanatakiwa kuwa na mtazamo yakinifu katika kulinda AMANI ya
nchi yetu kutokana na nchi zote zinazotuzunguka kuwa katika hali isiyolidhisha
kiamani na kimbilio lao ni katika nchi nchi yetu.Je taifa letu likikosa amani
tutakimbilia wapi ili tuitwe wakimbizi?
Kwa
wale wafuatiliaji wa vyombo vya habari wakubali kuwa kuna ukiukwaji mkubwa
katika Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuweka na
kuendeleza misingi ya utawala bora.
Kunaonekana
na kuwepo kwa upindishwaji wa haki za binadamu, demokrasia na utawala bora wa
sheria katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, Uganda,
Burundi na Rwanda), na misingi hiyo yote imepewa kipaumbele sana katika nchi
hizi.
Hata
hivyo nchi yetu imeshawahi kuingia katika mgongano mara kadhaa na nchi hizo
zote, hata ambazo azipo katika jumuiya ya Afrika Mashariki ila ni majirani
zetu, mafano Nchi ya Malawi na Tanzania waliingia katika mgogoro wa juu ya
umiliki wa ziwa nyassa na hadi sasa hakujapatiwa ufumuzi juu ya mgogoro huo
japo kwa sasa hali ni shwari.
Pia
Rais wa nchi ya Tanzania Jkaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa nchini
Rwanda, vyombo vyingi vya habari hapa nchini na huko Rwanda viliwahi kuripoti kuwa
wakuu hao waliingia katika hali isiyokuwa ya kawaida kila mmoja akimtunishia
mwenzake kifua japo nalo lilikwisha.
Deus
Kibambaamaye ni mtafiti na mchambuzi wa jamii aliyebobea katika maeneo ya
uhusiano wa kimataifa, katika moja ya maandishi yake aliwahi kusema kuwa:
“kutokana
na ufinyu wa malengo ya ujenzi wa utamanduni wa kidemokrasia katika Afrika
Mashariki, ukanda huu unaongoza kwa migogoro ya kisiasa ndani na baina ya
wanachama kiasi kwamba upo wakati inabidi kujaribu kutumia akili ya kuzaliwa katika
kutatua tafrani zinazojitokea kwa kukosa mfumo madhubuti ndani ya Mkataba wa
ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika mashariki wa mwaka 2000”
“kwa
bahati mbaya, pasipo demokrasia na utawala wa sheria katika nchi wanachama na
miongoni mwao, ushirikiano katika Nyanja nyinginezo unakuwa si endelevu na
unakuwa unapata tafrani kiasi cha kutikiswa na mawimbi ya utawala wa kibabe
kama ilivyotokea wakati wa Nduli Iddi Amin Dada mwishoni mwa miaka ya 1970s hadi
kugeuza lengo la ushirikiano la jumuiya”
Nyumba
yenye AMANI, UTULIVU NA UPENDO ndiyo inayokuwa na wageni kila mara, vivyo hivyo
katika nchi wawekezaji hupenda nchi yenye sifa za namna hii.
Post a Comment