NA,
YOHANA CHALLE
Jiji la Arusha limeendelea kuwa kinara katika
mchezo wa tenisi baada ya wachezaji wake kuibuka kidedea kwa kutwaa ushindi
katika umri tofauti tofauti,kwa mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya
Arusha Tenisi gymkhana klabu.
Mashindano hayo yalidhaminiwa na Jubilee tyres
ikiwa ni mwaka wa tatu sasa, huku yakishirikisha jumla ya wachezaji 90 ambao 28
kati yao ni wasichana kutoka Dar es salaam gymkhana klabu,Kijitonyama tenisi
klabu kutoka Dar es salaam,Morogoro tenisi klabu, ISM –Moshi campus, AICC klabu
–Arusha pamoja na Arusha tenis gymkhana klabu.
Katika umri wa miaka 6 kwa wasichana Schaefer
Swantje kutoka ISM Moshi campus alifuatiwa na Suhana Patel kutoka Arusha
gymkhana klabu,huku kwa upande wa wavulana wa umri huo Sahil Shah kutoka
ISM moshi campus na kufuatiwa na Yuvraj Sidhu kutoka Arusha gymkhana klabu.
Wasichana walio na umri wa miaka 8 Asha Ali
aliibuka mshindi na nafasi ya pili kumwendea Bahati Mdee wachezaji wote kutoka
klabu ya AICC na kwa upande wa wavulana mika 8 Johnson Peter alibuka mshindi na
kufuatiwa na Yasin Yusuph wote kutoka klabu ya AICC na kwa wasichana walio na
umri wa miaka 10 Vanessa Emmanuel kutoka AICC aliibuka kidedea na kufuatiwa na
Caroline Mwangata wa ISM Moshi campus,
kwa wavulana miaka hiyo Rashid Abdallah kutoka
Arusha gymkhana klabu na kufuatiwa na Abdumarik Kudra kutoka Morogoro klabu.
Kwa umri wa miaka 12 wasichana Shana
Martin aliongoza na kufuatiwa na Fei Amon wote kutoka Arusha gymkhana
klabu na wavulana Damas Felex na nafasi ya pili kumwendea Benjamini Laurance
wote kutoka AICC.
Huku kwa umri wa miaka 14 kwa wasichana
Jackline Kayuga kutoka kijitonyama Tenisi klabu na nafsi ya pili Anikaa
Aggarwal kutoka Arusha Gymkhana klabu na kwa wavulana wa umri huo
Deogratius Felex na kufuatiwa na Yusufu Laurance wote kutoka AICC.
Jackline Kayuga kutoka Kijitonyama
Tennis klabu alishika nafasi ya kwanzana kufuatiwa Hawa Yahya kutoka Dar es
salaam gymkhana klabu katika umri wa miaka 16 kwa wasichana na
kwa wavulana Omari Sulle Arusha Gymkhana klabu na kufuatiwa na Hassan
Hamisi - AICC Club Arusha.
Kwa upande wa umri wa miaka 18 kwa wasichana
hawakuwepo ,na walicheza wavulana pekee ambapo Emmanuel Mallya- Arusha Gymkhana
Club alifuatiwa na - Frank Menard -Arusha Gymkhana Club.
Nicholaus Leringa Kocha mkuu wa klabu ya
AGC alisema kuwa mashindano hayo hufanyika kila mwaka yakiwa na
lengo la kuwaimarisha vijana katika dhana nzima ya kunyanyua vipaji
vyao
Post a Comment