Mgeni
rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge (wa pili kushoto)
akiwasili kwenye kijiji cha Marua kata Kiruavunjo, mkoani Kilimanjaro
kwa ajili kupanda miti ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya
miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na kupokelewa na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa
Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto).(Pichazote na
Zainul Mzige wa modewjiblog).
*Sehemu ya Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa
Na Mwandishi wetu, Moshi
MASHIRIKA
ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yameadhimisha miaka 70 ya kuundwa
kwa umoja huo kwa kupanda zaidi ya 2000 katika miteremko ya mlima
Kilimanjaro.
Kazi
ya kupanda miti ilifanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau
wao ikiwemo serikali ya Tanzania pamoja na wanakijiji.
Kazi
ya kupanda miti iliongozwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez akishirikiana na Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi
ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge.
Shughuli hizo za kupanda miti zilifanyika katika kijiji cha Maruwa.
Akizungumza
wakati wa shughuli hiyo Waziri Mahenge alisema kwamba amefurahishwa na
hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 70 kwa
kuwakumbusha washirika wao wa maendeleo suala la mazingira.
“Ni
kawaida kuadhimisha kuundwa kwa Umoja wa Mataifa Oktoba 24 kila mwaka.
Mwaka huu ni tofauti na zaidi ya tofauti umekuwa maalumu kwa namna yake
kwa kuwa tunaadhimisha miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.” alisema
Waziri Mahenge.
Balozi
wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan akiwasili kwenye
sherehe ya kupanda miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na kusalimiana na Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
Hata
hivyo alikumbusha kwamba wakati tunaadhimisha miaka 70 ni vyema wadau
wa maendeleo wakaangalia historia na kujipanga kimkakati katika kusonga
mbele kimaendeleo kwa kujali mazingira.
Alisema
kwamba pamoja na hoja ya kujali mazingira pia serikali itaendelea
kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mambo mbalimbali ya
maendeleo.
Akizungumzia
umuhimu wa siku hiyo ya kupanda miti, Rodriguez, alisema kauli mbiu ya
wa mwaka huu ni “Sayari Moja Watu Bilioni 7: Utunzaji Mazingira ni
Wajibu Wetu”, umerandana na shughuli hizo za upandaji miti.
Alisema
kitendo cha upandaji miti kunaonesha wajibu wa kwanza wa kuhami
mazingira ya sayari yetu kwa manufaa ya kizazi kijacho cha wanadamu.
Alisema
mabadiliko ya tabia nchi si utani yapo kweli na ipo haja ya kuendelea
kuwapo kwa juhudi za makusudi za wakazi wa dunia hii kulinda mazingira
kwa ajili ya amani maendeleo na ustawi.
Mgeni
rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akisoma hotuba kwa
niaba ya Makamu wa Rais kwenye sherehe za upandaji miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Kwa
upande wake balozi wa Ulaya alisema upandaji miti katika mteremko wa
mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ni alama
muhimu katika mapambano ya wanadamu kulinda mazingira.
Alisema
ishara hiyo muhimu inaelekeza Umoja huo na wadau wake wa maendeleo
kuchukua tahadhari za kutosha kulinda mazingira na inakwenda sanjari na
malengo endelevu ya milennia (SDGs) ambayo yana mada tano za kuangaliwa
katika mazingira kuliko yale ya awali ambayo yalikuwa na mada moja tu.
Msemaji
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu alisema kwamba upandaji
miti uliofanyika ni moja ya shughuli kadhaa zitakazofanywa na Umoja huo
kuadhimisha miaka 70 toka kuanzishwa kwake.
Shughuli nyingine itakayofanywa ni kusafisha soko la Temeke, mashindano ya uchoraji kwa vijana na maadhimisho ya siku yenyewe.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa
Mataifa katika sherehe ya upandaji miti kwenye kijiji cha Marua ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika
mkoani Kilimanjaro.
Mkuu
wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Balozi Filiberto Sebregondi akizungumza
kwenye sherehe ya upandaji miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika mkoani
Kilimanjaro.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Afisa Tawala Mkuu
katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya wakifuatilia
hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye sherehe hizo.
Wakufunzi
kutoka chuo cha Ualimu Moshi wakitoa burudani kwenye hafla ya kupanda
miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70
ya Umoja wa Mataifa.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wanakijiji
wa kijiji cha Marua walioshiriki sherehe za upandaji miti ikiwa ni
Shamra shamra ya kusheherekea miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mgeni
rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akipanda mti katika
kijiji cha Marua karibu na miteremko ya mlima Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipanda mti katika kijiji cha
Marua mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya
Umoja wa Mataifa, kila mti unaashiria kila mwaka ambapo Umoja wa
Mataifa umekuwa ukileta maendeleo duniani ikiwemo kukabiliana na
mabadiliko ya Tabianchi. Kushoto ni Mshehereshaji Afisa Misitu wa mkoa
wa Kilimanjaro, Emanuel Kiyengi.
Afisa
Misitu wa mkoa wa Kilimanjaro, Emanuel Kiyengi (kulia) akitoa maelezo
kwa mgeni rasmi, mabalozi na viongozi wa serikali katika eneo maalum
lililotengwa kwa ajili ya kupanda miti 200 zoezi lililoendeshwa na Umoja
wa Mataifa nchini katika kusheherekea miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Mgeni
rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akiteta jambo
na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Mgeni
rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge (wa tatu kushoto)
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa eneo maalum lililotengwa kwa ajili
ya kupanda miti 2000 katika kijiji cha Marua karibu na miteremko
ya mlima Kilimanjaro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto), Mkuu wa ofisi ya
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto), Mkuu wa mabalozi,
ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma
Halfan Mpango (wa nne kushoto), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi
Fionnuala Gilsenan (wa tano kushoto), Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya,
Balozi Filiberto Sebregondi (wa nne kulia), Mkuu wa wilaya ya
Moshi, Novatus Makunga ( wa tatu kulia), Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Celestine Mushy ( wa pili kulia) pamoja na Afisa
Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya.
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akishiriki zoezi la kupanda miti katika kijiji cha Marua.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) akitoa
maelekezo kwa Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues (kulia) wakati wa zoezi la upandaji miti.
Mkuu
wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akishindilia udongo
kwenye mti aliopanda katika eneo lake.
Kaimu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP),
Titus Osundina akishiriki zoezi la upandaji miti katika kijiji cha Marua
mkoani Kilimanjaro.
Balozi
wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan akishiriki zoezi la
kupanda miti lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya
kusheherekea miaka 70 tangu kuanzishwa kwake duniani.
Afisa
Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akishiriki zoezi la kupanda mti katika kijiji cha Marua.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem na Beatrice
Mkiramweni kutoka ofisi za Mratibu Mkazi wa UN Tanzania wakipanda picha
ya kumbukumbu kwenye mti walioshirikiana kupanda.
Wakinamama
wa kijiji cha Marua wakipozi miti yao wakati wakielekea kuunga mkono
juhudu za Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya
Tabianchi.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana
mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakitazama
jambo na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues wakati wa zoezi
la kupanda miti katika miteremko ya mlima Kilimanjaro kijiji cha Marua mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Umoja wa Mataifa wakijadiliana jambo na mshehereshaji wa hafla hiyo.
Mgeni
rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akikata utepe kuzindua
jiwe la kumbukumbu la miaka 70 ya Umoja wa Mataifa kwenye eneo maalum
lililopandwa miti 2000 katika kijiji cha Marua, mkoani Kilimanjaro.
Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (kulia), mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania pamoja na
viongozi mbalimbali wa Serikali.
Zoezi la uzinduzi likiendelea.
Mgeni
rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akisoma maneno
yaliyoandikwa kwenye jiwe la kumbukumbu la miaka 70 ya Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania.
Mgeni
rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa
Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge katika picha ya pamoja
na mabalozi waalikwa, viongozi wa Serikali na wakuu wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa Tanzania.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mgeni rasmi.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akipata picha ya kumbukumbu na
wanakijiji wa kijiji cha Marua.
Post a Comment