Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) akikanusha kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua kampeni zake siku ya
tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam. Kanusho hilo lilitolewa
katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka Serikalini kuhusu Chadema kutumia Uwanja wa Taifa kuzindua kampeni zake siku ya
tarehe 22 Agosti, 2015 jijini Dar es Salaam. Kanusho hilo lilitolewa
katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) uliopo jijini Dar es Salaam.
Na Benedict Liwenga, MAELEZO.
SERIKALI
imekanusha taarifa zilizojitokeza kwenye Vyombo vya habari yakiwemo
magazeti na mitandao ya kijamii kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kitafanya mkutano hadhara Uwanja wa Taifa Dar es Salaam
tarehe 22 Agosti, 2015.
Akizungumza
na vyombo vya habari jana, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),
Assah Mwambene alisema serikali haijatoa ruhusa kwa chama chochote cha
siasa kutumia uwanja wa taifa kwa ajili ya shughuli za kisiasa.
Alikiri
kwamba ni kweli kwamba CHADEMA waliiandikia Wizara tarehe 12 Agosti,
2015 kutaka kutumia uwanja wa taifa katika uzinduzi wa kampeni lakini
ombi lao lilikataliwa kwa maelezo kwamba uwanja ule kwa mazingira ya
sasa hauruhusiwi kutumika kwa ajili ya mihadhara ya vyama vya siasa.
“kwa
kipindi haturuhusu uwanja wa taifa kutumika kwa mihadhara ya kampeni za
vyama vya siasa. Uamuzi huu unalenga kuweka uwanja katika mazingira
rafiki ya michezo na kuepuka athari zozote zinazoweza kujitokeza
kutokana na mihemuko ya kisiasa” alisema Bwana Mwambene.
Mwambene
ameeleza kuwa, Serikali imeamua uwanja huo ubaki kwa ajili ya kufanyia
shughuli zake za msingi za kimichezo ili kuepuka mihemuko na athari
yoyote inayoweza kujitokeza kutokana na hamasa za kisiasa.
“Ni
kweli kwamba tulipata barua ya Chadema kuomba Uwanja kutumika kwa ajili
ya mhadhara ya kisiasa wa CHADEMA hasa kuzindua Kampeni zao kwenye
Uwanja tayari tumeshawaandikia kuwaarifu kuwa Uwanja ule hauwezi
kutumika kwa ajili ya shughuli zozote za kisiasa” alisema Bwana
Mwambene.
Alisema vyama vyovyote vitakavyoomba kutumia Uwanja ule kwa shughuli za kisiasa havitaruhusiwa.
Post a Comment