Balozi
wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala Gilsenan, akizungumzia kuhusu
ufadhili kwa Watanzania wanaokwenda vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya
nchi. Sherehe hizo zimefanyika Alhamisi, Agosti 20, 2015 kwenye ofisi
za ubalozi huo Masaki jijini Dar es Salaam. (Picha na habari na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).
Baadhi ya wanufaika wa ufadhili huo wakimsikiliza Balozi wa Ireland (hayuko pichani).
Baadhi ya wafanyakazi na wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Gilsenan.
Deogratias
Gabriel Rugarabamu, Ofisa Tabibu wa Wilaya ya Kilindi, akipokea cheti
cha shukrani baada ya kuhitimu shahada ya uzamili ya Medical Entomology and Clinical Parasitology katika Chuo Kikuu cha Tumaini, KCMC .
Balozi Fionnuala Gilsenan wa Ireland akimpongeza Rubea
Mohammed Ali, Mkuu wa Idara katika Wizara ya Kilimo na Maliasili,
Zanzibar baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha
Sokoine katika Elimu ya Kilimo na Ushauri (Agricultural Education and
Extension).
David
Eliatosha Lekei, Ofisa Kilimo Wilaya ya Hai akipokea cheti cha shukrani
kutoka kwa Balozi wa Ireland nchini, Bi.Fionnuala Gilsenan baada ya
kuhitimu shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine katika Elimu
ya Kilimo na Ushauri (Agricultural Education and Extension).
Mshereheshaji akisoma majina ya wanufaika.
Stella
Zakayo Munisi, Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Sikika,
akipokea hati ya ufadhili kwenda kusomea shahada ya uzamili kuhusu
Organizational Development and Change katika Chuo Kikuu cha Dublin,
Ireland.
Na Daniel Mbega
SERIKALI
ya Ireland kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania, leo Agosti 20, 2015
imekabidhi scholarship kwa Watanzania 14 ambao watakwenda kusomea kozi
mbalimbali za shahada ya uzamili (masters) ambapo wanne kati yao
wakienda kusoma vyuo vikuu nchini Ireland.
Akikabidhi
hati hizo za ufadhili wa masomo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi.
Fionnuala Gilsenan, alisema utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wataalamu
mbalimbali ni jambo la msingi kutokana na ukweli kwamba ujuzi
watakaoupata unaweza kuliletea taifa maendeleo.
“Ufadhili
huu ni sehemu ya Mpango wa Mafunzo wa Kila Mwaka (Fellowship Training
Programme), katika sukuma mbele maendeleo ya nchi washirika wetu,
tunadhani tunao wajibu wa kusaidia pia kuwaelimisha watalaamu wao,”
alisema.
Aliwataja
wanufaika wanne waliobahatika kwenda ng’ambo kuwa ni Stella Zakayo
Munisi, Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Shirika la Sikika, ambaye
anakwenda kusomea shahada ya uzamili (Organizational Development and
Change) na Cosmas Joseph Mworia, Ofisa Ushirika na Ofisa Ufuatiliaji na
Ukadiriaji katika Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya Kondoa anayekwenda
kusomea shahada ya uzamili katika Kilimo Endelevu na Maendeleo Vijijini
(Sustainable Agriculture and Rural Development). Wawili hao wanakwenda
katika Chuo Kikuu cha Dublin.
Flavian
Majenga Lihwa, Mratibu Programu ya Elimu wa Shirika la Care Tanzania
yeye anakwenda Chuo Kikuu cha Dublin Institute of Technology kuchukua
shahada ya uzamili katika Maendeleo Endelevu (Sustainable Development)
na Zabron Elias Masatu, Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) ya Misenyi yeye
anakwenda Chuo Kikuu cha Taifa cha Ireland Maynooth (NUIM) kuchukua
shahada ya uzamili ya Immunolojia na Afya (Immunology and Global
Health).
Wanufaika
wengine 10 wa mwaka huu, kozi na vyuo wanavyokwenda vikiwa kwenye
mabano ni, Siwajibu Ally Selemani Malenge, Kaimu Ofisa
Kilimo/Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Kigoma (Chuo Kikuu cha
Sokoine – Elimu ya Kilimo na Ushauri ‘Agricultural Education and
Extension’); Edita Byangwamu Rutatora Kokwijuka, Ofisa Kilimo Daraja la
Kwanza kutoka Wilaya ya Muheza (Chuo Kikuu cha Sokoine – Kilimo); Doreen
Elias Mangesho, Mhasibu Mkuu wa CCBRT (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam –
Utawala wa Fedha); Elinlaa Michael Kivaya, Mchumi wa Kilimo wa Wilaya ya
Ngorongoro (Chuo Kikuu cha Sokoine – Kilimo na Uchumi Mtambuka
‘Agriculture and Applied Economics’); na Joshua Julius Musimu, Mkufunzi
wa Kilimo Daraja la Pili kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
(Chuo Kikuu cha Sokoine – Uchumi wa Kilimo ‘Agricultural Economics’).
Wengine
ni Fredrick Pius Massawe, Ofisa Kilimo Daraja la Kwanza kutoka Ofisi ya
Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro (Chuo Kikuu cha Sokoine –Kilimo);
Samuel Korinja Olekao, Mratibu wa Kinnapa Development Programme (Chuo
Kikuu cha Sokoine – Utunzaji wa Maliasili na Kilimo Endelevu); Eva
Emmanuel Mbambale, Ofisa Program wa Sikika (Chuo Kikuu cha
Makerere,Uganda – Afya ya Jamii); Iddi Alfani Shekabugi, Mchumi Daraja
la Kwanza katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika (Chuo Kikuu cha
Mzumbe – Uchumi na Fedha kwa Maendeleo); na Felix Lyope Lubuga, Ofisa
Utafiti wa Taasisi ya Afya Ifakara (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Afya
ya Jamii).
Awali, Balozi Fionnuala aliwatunuku vyeti wanufaika wengine 10 waliomaliza mwaka 2013 na 2014 katika fani mbalimbali.
Hao
ni Deogratias Gabriel Rugarabamu, Ofisa Tabibu wa Wilaya ya Kilindi
(Chuo Kikuu cha Tumaini, KCMC – Medical Entomology and Clinical
Parasitology); Pudensiana Clement Panga, Ofisa Uvuvi kutoka Wizara ya
Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi (Chuo Kikuu cha Sokoine – Sayansi ya
Chakula); Fatma Ally Mwasola Libaba, Ofisa Utafiti (Lishe) kutoka
Taasisi ya Chakula na Lishe (Chuo Kikuu cha Sokoine – lishe ya
Binadamu); Rubea Mohammed Ali, Mkuu wa Idara katika Wizara ya Kilimo na
Maliasili, Zanzibar (Chuo Kikuu cha Sokoine – Elimu ya Kilimo na Ushauri
‘Agricultural Education and Extension’); na David Eliatosha Lekei,
Ofisa Kilimo Wilaya ya Hai (Chuo Kikuu cha Sokoine – Elimu ya Kilimo na
Ushauri ‘Agricultural Education and Extension’).
Wengine
waliohitimu mwaka 2014 ni John Nobert Kirway, Mkufunzi Mkuu wa Mifugo
wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Arusha (Chuo Kikuu cha
Sokoine –Tropical Animal Production); Teddy Frederick Dionis Mamboleo,
Ofisa Utafiti (Lishe) kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (Chuo Kikuu cha
Sokoine – Lishe ya Binadamu); Adam Khamis Haji, Ofisa Mipango na
Utawala, Wizara ya Kilimo na Maliasili, Zanzibar (Chuo Kikuu cha Sokoine
– Maendeleo Vijijini); Jacob Polycarp Ngowi, Mkufunzi wa Masuala ya
Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi (Chuo Kikuu cha
Sokoine –Tropical Animal Production); na Mussa Said Bakari, Meneja wa
Maeneo Tengefu – Pemba kutoka Wizara ya Kilimo na Maliasili, Zanzibar
(Chuo Kikuu cha Sokoine – Utunzaji wa Maliasili na Kilimo Endelevu).
Mpango
huo wa Mafunzo wa kila Mwaka unahusisha Mfuko wa Misaada wa Ireland
(Irish Aid) kupitia program ya maendeleo ya Ubalozi huo nchini Tanzania.
Wanufaika
wa mpango huo wameteuliwa na washirika wa maendeleo wa Ireland nchini
Tanzania, zikiwemo wizara mbalimbali za Serikali, halmashauri za wilaya
na mashirika yasiyo ya kiserikali, ambayo shughuli zao zinawiana na
maeneo ya vipaumbele vya Irish Aid, hususan Kilimo, Afya, Lishe na
Utawala.
Aidha,
wanufaika wote ni watendaji wa kati ambao baada ya kuhitimu masomo yao
watarejea kwenye mashirika na taasisi zao kutumia ujuzi walioupata kwa
manufaa ya jamii.
“Kwa
wanufaika watakaokwenda kusoma nchini Ireland, program inatoa fursa
nzuri ya kujifunza katika hadhi ya kimataifa na kunufaika na hazina
kubwa ya nyenzo za tafiti zinazotolewa kwenye Vyuo Vikuu na Taasisi za
Teknolojia za Ireland,” amesisitiza Balozi Fionnuala.
Akaongeza:
“Inatarajiwa kwamba mafunzo ya wataalamu hawa yatachangia kwa kiasi
kikubwa maendeleo ya Tanzania, na kuendelea kuimarisha ushirika wa
kielimu baina ya Ireland na Tanzania.”
Ireland,
kupitia Mfuko wa Misaada (Irish Aid), imekuwa ikidhamini Mpango huo wa
Mafunzo nchini Tanzania kwa miaka 40 sasa ambapo program hiyo imekuwa
msingi wa msaada katika kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea na inaendana
na mkakati wa kupunguza umaskini wa nchi washirika wa Ireland, hasa
lengo likiwa kuwapatia wataalamu elimu ya juu ili waendeleze taasisi
zao.
Post a Comment