BALOZI SEIF ALAANI VIKALI VITENDO VYA UGAIDI NA UTEKAJI WA WATOTO WA KIKE
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd ameungana na
Majaji wanawake Duniani, kulaani vikali kitendo cha Ugaidi cha utekaji
watoto wa kike 200 wa Nigeria, kilichofanywa hivi karibuni.
Hayo aliyasema jana wakati akifunga mkutano wa 12, uliofanyika Jijini
Arusha na kukutanisha Majaji wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani
(IAWJ) kujadili changamoto wanazokumbana nazo wakati wa utekelezaji wa
kazi zao.
Alisema kuwa kimsingi Duniani kuna unyanyasaji ambao unaendelea
kufanyika dhidi ya wanawake na watoto, hali ambayo Majaji wanawake
wamekuwa mstari w ambele kupambana nao.
“Lakini mimi nawaunga mkono nanyi katika maadhimio yenu ya kupinga
ukatili huu wa utekeaji wa toto wetu huko Nigeria, siyo ubinadamu na
inapaswa kulaaniwa na kila mmoja,”alisema.
Aidha alisema Majaji wanawake wamekuwa mstari w ambele kufanya kazi
zao kwa uadilifu na kuhakikisha haki inapatikana bila ubaguzi kwa kila
mtu.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Majaji wanawake Tanzania, (TAWJA), Jaji
Engera Kileo, alisema katika mkutano huo wa siku nne, wameadhimia
mambo mengi, ilakubwa ni azimio la kulaani kitendo cha wasichana wa
Nigeria kutekwa ambao kimsingi hawana makosa yoyote ya kufanyiw
aukatili huo.
“Hawa wasichana tunawalaani waliowafanyia hivyo, sababu wanakosa haki
yao ya msingi ya kuwa huru na tunaomba matatifa makubwa na Umoja wa
Mataifa, vikiwemo vyombo vyao kuingilia sakata hili ili watoto hao
wapatikane wawe huru,”alisema.
Alisema hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu atafurahia kitendo hicho
cha kigaidi na kinapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na mataifa yote
Duniani. Katika Mkutano huo pia wajumbe walifanya uchaguzi na walimchaguaRaisi wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani (IAWJ), Teresita Leonardo, ambaye anachukua nafasi ya aliyekuwa Raisi wa chama hicho EusebiaMunuo wa Tanzania
Post a Comment