Mwanamama akivuka katika kivuko cha mnepo cha Kiyungi
Viongozi na wataalamu wakijadili jinsi ya kuimarisha kivuko cha Mnepo cha Kiyungi
Diwani wa kata ya Machame Weruweru Adris Mandrai akipita katika kivuko cha mnepo cha Kiyungi |
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga wa pili kutoka mbele akiwa na Afisa mtendaji
mkuu wa kiwanda cha TPC,,Jaffari Ally(Mbele) na diwani wa kata ya
Machame Weruweru,Adris Mandrai baada ya kukagua daraja la Mnepo la
Kiyungi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ametembelea kivuko cha Kiyungi
kinachofahamika kama daraja la Mnepo kinachounganisha wilaya ya Hai na
Moshi ambacho sasa hivi kipo katika hali mbaya zaidi kutokana na mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha na kuahidi kitaanza kufanyiwa ukarabati wa
dhararu Jumamosi ijayo angalau kiweze kutumika wakati zinasubiriwa fedha
za ujenzi wa kivuko kipya.Ameeleza kuwa kampuni ya Sukari ya TPC
imekubali kutoa baadhi ya vifaa vya ukarabati.
Post a Comment