Amebainisha kuwa, Jeshi hilo kwa kushirikiana na Baraza la Mtihani la Taifa (NECTA), walifanya zoezi la uhakiki wa vyeti vya wanafunzi hao ndipo ilipo bainika kuwa wanafunzi 212 kati ya wanafunzi 3,390 waligushi vyeti vya elimu ya sekondari kwa lengo la kujiunga na Jeshi hilo.
Andengenye, amesema kufuatia hali hiyo Jeshi hilo nchini, limewaachisha mafunzo ya ‘uaskari’ wananfunzi hao ili hatua nyingine za kiupelelezi ziendeleee kuchukuliwa kwa kushirikiana na taasisi nyingine zinazohusika.
Amesema ili kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea kuwa na ‘Askari’ wenye weledi na uamifu kwa raia na taifa kwa ujumla, wataelenda kufanya uhakiki wa vyeti kwa wanafunzi wote ili kuwabaini wale wote wanao gushi vyeti.
“Itambulike kuwa kitendo chochote cha kugushi ni kosa la jinai na pindi mtu anapobainika kufanya hivyo Jeshi la Polisi, halitasita kuwachukulia hatua za kisheria” alisema Andengenye.
Alitumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kuacha tabia ya kugushi vyeti au kutumia vyeti ambavyo si halali, na badala yake wafuate taratibu na sheria zilizopo kwa ustawi wa Taifa.
Jumla ya wanafunzi 3,415 waliripoti katika chuo hicho Desemba 10 mwaka 2013, wanafunzi wa mafunzo ya uaskari 25 waliachishwa mafunzo na kufanya idada hiyo kupungua na kufikia wanafunzi 3,390, kutokana na matatizo ya kiafya na makosa ya Kinidhamu.
Post a Comment