PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAPOKEZI YA LEMA KIA YAFUNIKA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya wakina Mama wakiiimba nyimbo za kumsifia Lema   Baadhi ya VIJANA WA chama hicho wakiiimba nyimbo za kumpongeza Lema Askari POLISI ...

Baadhi ya wakina Mama wakiiimba nyimbo za kumsifia Lema

 

Baadhi ya VIJANA WA chama hicho wakiiimba nyimbo za kumpongeza Lema

Askari POLISI wakihakikisha usalama unakuwepo Muda wote


Na; Mwandishi wetu, KIA

maipacarusha20@gmail.com

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Arusha mjini kupitia Chadema, Godbless Lema hatimaye amerejea nchini, akitokea uhamishoni nchini Canada na amepokewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro na viongozi kadhaa wa Chadema na Viongozi wa dini.

Lema baada ya kushuka katika ndege ya shirika la Ethiopian alielekezwa moja kwa moja chumba Cha wageni maarufu(VIP) na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.

Baadae Lema  alifanya mazungumzo kidogo na viongozi wa chadema na Sasa msafara umeanza kuelekea Arusha.

Lema aliwasalimia viongozi wote waliofika kumpokea na amewapungia mkono mamia ya wanachadema waliokuwa nje ya VIP vikiwepo vikundi kadhaa vya Ngoma.

Ikumbukwe Lema aliondoka nchini mara baada ya uchaguzi Mkuu mwaka 2020 Ili kuokoa maisha yake kwa kile ambacho ameeleza kupokea vitisho vya kisiasa.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top