PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MKUU WA WILAYA KIBAHA NICKSON AWATAKA WALIMU KUONGEZA UFAULU WA WANAFUNZI WILAYANI HAPO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon akizungumza katika kongamano la Elimu Kibaha.   NA: JULIETH ...

MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon

MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon akizungumza katika kongamano la Elimu Kibaha.

 


NA: JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA 


maipacarusha20@gmail.com 


MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimon amesema ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi katika shule za wilaya hiyo kila mwalimu anatakiwa kuhakikisha kwenye somo lake kuna ufaulu wa alama C.


Aidha Mkuu wa shule ambaye ufaulu wa wanafunzi utakuwa chini ya alama C atashushwa daraja kwa kushindwa kuwasimamia vizuri walimu wake kwenye suala zima la ufundishaji.



Hayo yameelezwa mjini Kibaha wakati wa Kongamano la elimu ambalo lilishirikisha Maafisa Elimu Kata, wilaya na walimu wa kuu wa shule za Sekondari na za Msingi wa Halmashauri hiyo.



Saimon amesema kipimo cha mwalimu kitakuwa ni alama C na kwa mwalimu mkuu hivyo hivyo huku akisisitiza kuwa kila shule inatakiwa kuwa na mkakati wa kupima ufaulu utakaokuwa unaongozwa na Mwalimu wa taaluma na itakuwa inafanyika kila baada ya miezi mitatu.


Mkuu huyo wa Wilaya amesema walimu ambao masomo yao yatakuwa na ufaulu wa juu watapewa motisha wa viwanja pamoja na fedha ili waongeze juhudi kuinua ufaulu wa Wilaya hiyo.


"Kila mwalimu ahikikishe kuanzia Januari hadi Desemba mwanafunzi katika somo lake anapata ufaulu wa alama C, ziwepo kamati za ufuatiliaji shuleni zitakazoongozwa na Mwalimu wa taaluma na hizo zitakuwa zinasahihisha mitihani inayotolewa na kutoa tathmini" amesema.


Ameshauri pia kila shule kuona namna ya kutokomeza ziro kuanzia kidato cha kwanza na kwakufanya hivyo itaondoa kufeli wanafunzi wanapofika kidato cha nne.


Saimon amesema kwasasa asilimia 80 ya wanafunzi wanafeli masomo ya sayansi huku asilimia 50 wakifeli kidato cha nne jambo ambalo linashusha taaluma kwa Wilaya hiyo.


"Wilaya yetu ina viwanda vingi sasa hii hali ya kufeli masomo ya sayansi utasababisha waendelee kukosa ajira tunatakiwa kuweka mipango mikakati kukabiliana na hii hali kuongeza ufaulu kwa masomo yote na katika haya ya sayansi" amesema.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibaha mjini Mussa Ndomba amezielekeza kamati za uongozi za shule kushughulika na kero kwenye shule badala ya kusubiri Halmashauri izifanyie kazi.

Ndomba pia amesema walimu pia wanatakiwa kuweka msisitizo wa kufundisha masomo ya lugha za kigeni ili wahitimu waweze kuajirika kwenye kampuni zinazowekeza katika Wilaya ya Kibaha.


Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma Msingi, Adinani Livamba amesema wao kama Idara wamejipanga kuhakikisha Kibaha Mji inaendelea kufanya vizuri kitaaluma katika mitihani yote ya Kitaifa na Kimkoa.

Ameiomba Jamii kuendelee kushirikiana na Walimu na Serikali katika kuendelea kuinua kiwango cha Ufaulu Shuleni kwa kuhakikisha Wanafunzi wote Wanapata chakula cha mchana, kudhibiti utoro na kuongeza usimamizi wa nidhamu ya Wanafunzi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top