PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: CHAMA CHA WAPANDA MLIMA KILIMANJARO (TPO) CHAPATA VIONGOZI WAPYA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mmoja wa viongha wapagazi wa chama cha wapagazi akizungumza na wanachama wa chama hicho Katibu wa Bodi ya TPO, Mussa Juma akizungumza...
Mmoja wa viongha wapagazi wa chama cha wapagazi akizungumza na wanachama wa chama hicho

Katibu wa Bodi ya TPO, Mussa Juma akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo na wanachama wa chama cha wapagazi waliohudhuria katika uchaguzi huo

Baadhi ya wanachama wakisiliza kwa makini sera za wagombea waliokuwa wakijinadi na kuomba kura kwa wanachama hao
Image result for TANZANIA PORTERS ORGANIZATION
Baadhi ya porters wakiwajibika kuwasaidia watalii katika  mlima kilimanjaro


Image result for TANZANIA PORTERS ORGANIZATION
baadhi ya porters wakiwa wamepumzika

Mwandishi wetu, Moshi

Chama cha wapagazi wa Mlima Kilimanjaro(TPO), juzi kimechagua viongozi wapya, ambao wataongoza chama hicho kwa miaka mitatu.

Katika uchaguzi huo, uliofanyika ukumbi cha Umoja hosteli mjini Moshi kwa kusimamiwa na bodi ya chama hicho, Elibariki Sam alichaguliwa kuwa Mwenyekiti.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,ambao ulishirikisha viongozi kutoka kanda nne za Marangu, Machame, Arusha na Moshi, Katibu wa Bodi ya TPO, Mussa Juma jumla la kura zilizopigwa zilikuwa ni 19.

Alisema Sam alipata kura 8 akifatiwa na Lotang'amwaki  Mollel aliyepata kura 6, Hemedi Juma kura 4 na kura mbili ziliharibika huu mgombea Frank Mpunju akikosa kura baada ya kujitoa.

Juma alisema kwa mujibu wa taratibu cha TPO, Mollel alichaguliwa kushika nafasi ya makamu Mwenyekiti wa chama hicho.

Alisema viongozi hao, wataungana na secretarieti ya TPO, ambayo inaongozwa na Katibu Mtendaji Loshiye Mollel na viongozi wa wengine kutoka kanda ya Arusha, Marangu, Machame na Moshi.

Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa bodi wa chama hicho, Alex Lemunge aliwataka wapagazi kujiendeleza kielimu na ambao watashindwa  watakuwa wanajiondoa kufanyakazi hiyo.

Lemunge alisema, utaratibu wa kujiendeleza kielimu, umetolewa na wizara ya maliasili na Utalii, ili kuhakikisha watoa huduma wote kwa watalii wanakuwa na elimu na kusajiliwa.

Alisema tayari utaratibu wa kusoma umeanza kuwekwa baina ya TPO kwa kushirikiana na chuo cha Wanyamapori cha Mweka na wadau wengine, kuhakikisha wapagazi zaidi ya 20,000 wanapatiwa elimu juu ya kazi zao ili kupata sifa ya kufanyakazi hiyo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top