Benny Mwaipaja
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezindua zoezi la ukusanyaji
wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania
Bara mwaka 2017/2018, utakaogharimu shilingi bilioni 10 zilizotolewa na
Benki ya Dunia.
Lengo
la utafiti huo utakaofanywa na Ofisi Kuu ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni
kupata takwimu zinazohusu shughuli za kijamii na kiuchumi, mapato na
matumizi, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali katika ngazi ya kaya.
Dkt. Mpango alisema kuwa Utafiti
huo utaiwezesha Serikali kupima kiwango cha hali ya umaskini wa kipato,
chakula na pengo baina ya matajiri na maskini kuanzia kipindi cha
mwaka 2013 hadi sasa.
“Takwimu
zilizopo hivi sasa zinaonesha kwamba kiwango cha umasikini wa kipato
ulipungua kutoka asilimia 34 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 28.2 mwaka
2012” Alisema Dkt. Mpango.
Alisema
pamoja na takwimu hizo, bado kiwango cha umasikini ni kikubwa na kwamba
Serikali kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali inahakikisha
kuwa kila mwananchi anapata huduma za msingi za kijamii kwa kadri uchumi
unavyokua hivyo kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la umasikini.
“Nimefurahi
kuelezwa kuwa utafiti huu utakusanya takwimu katika kaya binafsi 10,460
kwa Tanzania Bara kuanzia Novemba 2017 hadi Novemba 2018 na kwamba
kupitia zoezi hili, Serikali ya Awamu ya Tano imetoa ajira kwa vijana
wapata 620 katika maeneo ya vijijini na mijini” alieleza Dkt. Mpango.
Aliwaasa
wadadisi hao kufanyakazi zao kwa umakini na weredi mkubwa ili takwimu
zitakazopatikana ziwe sahihi na kuonya kuwa Serikali haitasita
kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaojaribu kuvuruga zoezi
hili.
Awali,
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
alieleza kuwa ukusanyaji wa Takwimu za utafiti wa mapato na matumizi ya
kaya binafsi utafanyika katika maeneo 754 yaliyochaguliwa kitaalamu kwa
kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012.
“Utafiti
huu utakuwa wa saba tangu Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961, ambapo
tafuti nyngine zilifanyika 1969, 1991/92, 2001, 20117 na mwaka 2011/12”
aliongeza Dkt. Chuwa.
Alisema
kuwa utafiti huo mpya utafanyika kwa kutumia teknolojia ya kisasa
ijulikanayo kama Survey Solution (CAPI) na kwamba matokeo ya awali ya
utafiti huo yanatarajiwa kutolewa ndani ya miezi sita ijayo ili nchi
iweze kufahamu kiwango cha umasikini uliopo katika jamii hivi sasa baada
ya kufanyika kwa utafiti kama huo miaka mitano iliyopita.
“Utafiti
wa mwisho uliofanyika mwaka 2011/2012 uliotumia karatasi uligharimu
shilingi bilioni 20 lakini kwa kutumia teknolojia mpya, utafiti huu
utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 10 pekee” alisisitiza Dkt. Chuwa.
Dkt.
Chuwa alisema kuwa anaamini matokeo ya utafiti huo yatakuwa chachu ya
kupata takwimu za msingi kwa ajili ya kufuatilia na kutathimini
utekelezaji wa program mbalimbali za kitaifa na kimataifa zenye kulenga
kupunguza kiwango cha umasikini nchini.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu
ya TEHAMA Bw. Baltazar Kibola alisema kuwa watatoa ushirikiano
wakutosha kwa wadadisi hao katika ngazi zote kuanzia Mikoa, Wilaya,
Halmashauri, Kata, Vijiji na Vitongoji ikiwemo kufanyia marekebisho
vitendeakazi vya kukusanyia takwimu hizo vikipata hitililafu ili azma ya
Serikali ya kupata takwimu sahihi itimie kama ilivyopangwa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa
maelezo kuhusu namna utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi
utakavyotekelezwa wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa
wa zoezi la ukusanyaji takwimu za utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya
Binafsi, Mjini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kufunga
mafunzo ya Wadadisi, na kuzindua zoezi la ukusanyaji wa Takwimu za
Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka
2017/2018, Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza
jambo wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi na kuzindua zoezi la
ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi
Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma, utakaohusisha kaya binafsi
10,460.
Meza
Kuu (Walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na Wasimamizi wa zoezi la
ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi
Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma. Utafiti huo utahusisha kaya
binafsi 10,460.
Wadadisi
wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania
Bara wa Mwaka 2017/2018, wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla
ya uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa
maelezo kuhusu namna utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi
Tanzania Bara utakao gharimu shilingi bilioni 10, wakati wa kufunga
mafunzo ya wadadisi na uzinduzi wa wa zoezi la ukusanyaji takwimu za
utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi, Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza
jambo wakati wa kufunga mafunzo ya Wadadisi na kuzindua zoezi la
ukusanyaji wa Takwimu za Utafiti wa Mapato na Matumizi wa Kaya Binafsi
Tanzania Bara mwaka 2017/2018, mjini Dodoma, utakaohusisha kaya binafsi
10,460.
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI, anayeshughulikia TEHAMA
Bw. Baltazar Kibola, akieleza mikakati ya Ofisi yake katika kusaidia
kufanikisha zoezi la ukusanyaji wa takwimu za utafiti wa Mapato na
Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara mwaka 2017/2018, uzinduzi huo
umefanyika mjini Dodoma.
Post a Comment