GODBLESS LEMA akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo |
Na: Onesmo Mbise Arusha
Mwenyekiti Chadema Kanda Ya Kaskazini Godbless Lema Ametoa Kwa Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani Kuondoa Marufuku ya kutokuuza Madini Ya Tanzanite nje ya Mji Wa Mererani kwani Kufanya Hvyo ni kulifanya Soko la Tanzanite Kuzorota Hapa Nchini.
Lema Amesema hayo katika Mkutano wake na vyombo vya Habari Jijini Arusha ambapo Ameeleza Kuwa Kuuza Madini ya Tanzanite Katika Mjii wa Mererani Pekee ni kosa la Kimkakati la Kibiashara ambalo Linayafanya Madini ya Tanzanite yasiwe na thamani Kwa Watanzania.
Amesema kuwa ni wakati Sasa Serikali Kuruhusu Mfumo wa Biashara Kwa Madini Hayo kuwa Katika Soko Huria Ili Madini yapatikane Kwa wepesi Ndani na nje ya Nchi na Kwa kufanya Hvyo kutaongeza Soko na Uhitajio Wa Madini Hayo.
Aidha Ameitaka Serikali Kuangalia Namna Ya kuweka Mfumo wa kielectronikia utakao Saidia Kutambua Uhalali Madini ya Tanzanite Sokoni Ili kuepusha wizi au utoroshaji unaoweza kufanyika kiholela.
Lema Amebainisha Kuwa Mfumo wa Soko Huria katika Uuzaji wa Madini ya Tanzanite Utaongeza Mapato ya Serikali na hvyo kuchangia Ukuaji wa Uchumi wa Nchi ya Tanzania.
Pia Lema Amesema kuwa Arusha Ni Jiji la kitalii hvyo Serikali inapaswa Kuruhusu Biashara hyo Kufanyika Arusha mjini kupitia Broka ambao Wana leseni za Kufanya Biashara hyo Ili kuwezeshaji upatikanaji wake kwa wepesi.
Post a Comment