PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MLINZI WA CHUO AIBA GARI KWENYE MAEGESHO YA CHUO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  .       Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea ...

 


.      


Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa
.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa Habari juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani Iringa


Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia David Richard mwenye umri wa miaka 23 kwa kuiba gari aina ya raum rangi ya Grey yenye namba za usajili T 702 DFV mali ya Gasper Abraham mwenye umri wa miaka 34 aliloiba katika eneo lake la kazi

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa wamemkamata kijana huyo baada ya taarifa za kuibiwa kwa gari hilo kutolewa na hivyo kupelekea jeshi la polisi kufanya doria ya kutosha na kuikuta wilaya ya kilolo mkoani hapa

“Tunamshikilia David Richard mwenye umri wa miaka 23 mlinzi wa RUCU aliiba gari hiyo ikiwa kwenye maegesho lakini mmiliki alitoa taarifa kwenye jeshi la polisi na ndipo utaratibu wa kumtafuta ukaanza ndipo ilipokutwa kwa mtuhumiwa akiitumia wilaya ya kilolo “

Pamoja na hayo Allan Bukumbi alisema  kuwa  miongoni wa waharifu waliofanikiwa kuwakamata katika  msako walioufanya  walifanikiwa kumkamata ndugu Boni Kipalile kwa kosa la kukutwa na silaha aina ya shortgun yenye namba 14949 na risasi tatu moja ikiwa chemba huku wakimshikilia benadetha kipago umri wa miaka 61 akiwa na meno ya tembo na kiboko

“Ndugu waandishi wa habari kutokana na taarifa za siri kijiji cha kiponzero wilaya ya mkoa wa Iringa tulifanikiwa kumkamata boni kipalile mkulima mkazi wa igangidungu anayetuhumiwa kujihisuisha na matukio mbalimbali ya kihalifu akizwa na silaha moja aina ya shortgun namba za usajili 14949na risasi tatu moja ikiwa chemba pamoja na hilo tunamshikilia benedetha kipago kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo na meno mawili ya kiboko “

Aidha kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Iringa amewataka wananchi kujitokeza na kutambua mali zilizokamatwa kwa watuhumiwa Emmanuel Mnyeke (28) na Alfred Mkanula (25) ambao walikamatwa na mali za wizi ikiwa ni pamoja na pikipiki 6 aina ya sanlg ,boxer na honda

Katika kushighulikia changamoto mbalimbali jeshi la polisi mkoani iringa lilifanikiwa kumkamata Sebastian Mahuwili (42) aliyehukumiwa kwa kesi ya kubaka mtoto wa miaka 6 na hivyo kupelekea Kufungwa miaka 30 jela kutokana na ushahidi kukamilika

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top