PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: YANGA WAITANDIKA NAMUNGO FC BAO MBILI BILA NA KUJIKITA KILELENI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Yanick Bangla MVP wa ligi kuu akishangilia goli la kwanza alilowafunga Namungo Fc katika dakoka 40 ya mchezo huo  USHINDI wa 2-0 uliopata Ya...
Yanick Bangla MVP wa ligi kuu akishangilia goli la kwanza alilowafunga Namungo Fc katika dakoka 40 ya mchezo huo




 USHINDI wa 2-0 uliopata Yanga dhidi ya Namungo unaifanya timu hiyo ivunje mwiko wa kutopata ushindi katika uwanja wa Majaliwa

Tuisila Kisinda akishangilia goli la pili aliloifungia Yanga dakika ya 82 katika mchezo wao na Namungo 

Mabao ya Yanick Bangala dakika ya 40 na Tuisila Kisinda dakika ya 82 yametosha kuipa Yanga ipate ushindi wa kwanza kwenye Ligi Kuu katika uwanja huo.

Namungo na Yanga kwenye mechi sita za mwisho za Ligi Kuu zimecheza mechi tatu kwenye uwanja huo na zote zilimalizika kwa sare



Wakati huo kwenye mechi tatu walizocheza katika uwanja wa Mkapa, walitoka sare mbili na Yanga kushinda mchezo mmoja.

Mshambuliaji wa Yanga, Tuisila Kisinda amefunga bao lake la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu tangu arejee katika kikosi hicho akitoka kwa mkopo RS Berkane ya Morocco.



Matokeo hayo yanaifanya Yanga iendelee kukaa kileleni ikiwa na pointi 38, Azam FC 35, Simba 34 , Singida Big Stars 27 na Geita Gold ikifunga tano bora kwa pointi 22 baada ya timu zote kucheza mechi 15



Credit to Mwanaspoti

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top