PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: FRIEDKIN CONSERVATION FUND WATOA MILLIONI 84 KUSAIDIA MIRADI YA MAENDELEO KWA JAMII YA MOYOWOSI, UVINZA NA UGALA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Baadhi ya wakurugenzi na viongozi wa Friedkin Conservation Fund wakiwa katika maonesho ya nanenane mwaka huu mkoani Simiyu   Mwandish...
  Baadhi ya wakurugenzi na viongozi wa Friedkin Conservation Fund wakiwa katika maonesho ya nanenane mwaka huu mkoani Simiyu 
Mwandishi wetu,Arusha.
Taasisi ya uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), imetoa msaada wa zaidi ya  sh 84 milioni kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii ambayo inazunguka mapori ya akiba ya Moyowosi, Uvinza na Ugalla ili kujikwamua na umasikini.
Meneja Maendeleo ya jamii wa taasisi ya FCF yenye makao makuu jijini Arusha,  Nana Grosse-Woodley  alisema fedha hizo ni sehemu ya misaada ya kijamii ambayo imetolewa kati ya mwaka jana na mwaka huu katika eneo hilo ambapo taasisi hiyo, kupitia kampuni yake kitalii ya Wengert Windrose Safaris  iliyowekeza katika eneo hilo.
Grosse-Woodley alisema fedha,zimetolewa katika kusaidia vikundi vya ujasiriamali(VICOBA), kusaidia utengenezaji wa madawati 260,kuwatengenezea mizinga ya nyuki 130  wananchi na kugharamia kambi za matibabu kwa wananchi wa eneo hilo.
"misaada hii imekuwa na manufaa makubwa kwa jamii, kwani sasa baadhi wameweza kuanzisha miradi yao, wengine kupona maradhi na katika shule tumesaidia kupunguza tatizo la watoto kukaa chini kwa kukosa madawati"alisema.
Afisa Maendeleo ya jamii ya FCF katika pori la akiba la Moyowosi na Uvinza. Batro Ngilangwa alisema kampuni ya Wingert Windrose Safaris  ambayo ipo chini ya FCF, mwaka 2017 ilitumia kiasi cha sh 17.1milioni,katika kusaidia miradi ya jamii.
 Alisema katika eneo la pori la Myowosi vikundi vya vikoba viliwezesha kiasi cha sh 2.6 milioni, Wanafunzi walisaidia kulipiwa ada kiasi cha sh 1.5 milion na pia kiasi cha sh 1.7 kilitumika kukarabati darasa shule ya msingi Migezi.
"katika eneo la Uvinza mwaka  2017,FCF ilisaidia kulipia ada wanafunzi kiasi cha sh 1.2 milioni,ujenzi kiwanja cha michezo 1.8 milion na  vikundi vya ufugaji wa nyuki  vimenufaika na kiasi cha sh 9.9 milioni"alisema
Alisema katika eneo la pori la akiba la Ugalla Kusini na Kaskazini mwaka 2017  kiasi cha sh 23.5 milioni zilitolewa kuchangia miradi ya maendeleo.ikiwepo vikundi vya vikoba,ujenzi wa madarasa,ujenzi wa miradi ya uvunaji maji  ya mvua na udhamini wa wanafunzi.
Mapori hayo ya Akiba ambayo yapo chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya wanyamapori nchini(TAWA), pia kumeweza kutokomezwa matukio ya ujangili kutokana na ushirikiano mkubwa wa ulinzi baina ya askari wa TAWA, FCF na wananchi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top