Baadhi ya wafanyakazi wa Mobisol Wakifanya usafi wa mazingira jijini Arusha mapema leo |
Baadhi ya wafanyakazi wa Mobisol Wakifanya usafi wa mazingira jijini Arusha mapema leo |
Mwandishi wetu, Arusha.
Wakazi wa mkoa wa Arusha, wametakiwa kutumia nishati mbadala ya nguvu
za jua, ili kujiepusha na uchafu na uharibifu wa mazingira katika
maeneo yao.
Mkuu wa
kitengo cha masoko wa kampuni ya kimataifa ya Mobisol ,Seth Mathemu
alitoa wito huo katika maadhimisho ya siku ya usafi wa mazingira
duniani, ambayo wafanyakazi wa kampuni hiyo, waliadhimisha katika jiji
la Arusha kwa kufanya usafi.
Mathemu
alisema matumizi ya nishati mbadala yanaweza kusaidia sana, kupambana
na tatizo la uharibifu na uchafuzi wa mazingira katika maeneo mbali
mbali nchini.
"Suala la
ulinzi wa mazingira na afya za watu ni sehemu ya malengo makuu ya
kampuni ya Mobisol imeungana na mataifa 156 duniani kushiriki katika maadhimisho ya usafi wa mazingira na kutoa
misaada mbali mbali"alisema
Alisema Mobisol hadi sasa imeweza kuwaunganishia watu 500,000 umeme wa jua katika nchi za Afrika ya Mashariki.
Awali Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega
akizungumza katika maadhimisho hayo,alisema suala la usafi na uhifadhi wa mazingira linapaswa kuwa la kudumu hapa nchini.
Alisema
mkoa wa Arusha, umejipanga kuhakikisha unaendelea kuhifadhi mazingira
na hivyo suala la usafi litaendelea kuwa la kudumu.
Post a Comment