Mwandishi wetu,Arusha.
Vita
dhidi ya ujangili wa Faru, imeendelea kushika kasi na sasa Faru wa
serengeti,wataanza kulindwa na vifaa maalum vya kielekroniki katika
mradi ambao utagharimu zaidi ya shilingi 2.5 bilioni.
Mratibu
wa Mradi wa uhifadhi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti,
Philbert Ngoti alisema, vifaa hivyo ambavyo vitawezesha Faru wa
Serengeti kuwa salama zaidi.
Alisema
Faru wa Serengeti wanafungwa vifaa vya aina mbili,vya kielekroniki VHF
transmitter ambacho kinawezesha kuwafatilia walipo kila siku na pia
wanafungwa katika mguu wa kulia kifaa cha kisasa cha LoRa collar ambacho
pia kinafatilia na kuonesha mienendo yao kila siku.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii,Japhet Hasunga, alisema zoezi la
ufungwaji wa vifaa ya utambuzi na usalama kwa Faru ni muhimu sana katika
kuimarisha vita dhidi ya ujangili.
Alisema zoezi
hilo pia litasaidia kuongeza ufatiliaji wa faru,wanyama ambao wapo
hatarini kutoweka duniani na sasa kila siku watajulikana wapo wapi,
wanakula nini, wanaumwa ama wanamatatizo na hivyo kuchukuliwa hatua.
Meneja
miradi wa shirika la Frunkfurt Tanzania, Rian Habuschagne, alisema
katika mradi huo ambao ni mara ya kwanza kufanyika nchini, pia
kumejengwa minara ya mawasiliano katika maeneo yote ya mapito ya Faru.
Alisema
zoezi la kufungwa vifaa hivyo linasimamiwa na watafiti na wahifadhi
maarufu wa Faru barani Afrika, wakiongozwa na Pete Morkel na wanatarajia
Faru wote wa serengeti kufungwa vifaa hivyo.
"hili
zoezi linagharama kubwa tunawashukuru Friedkin Conservation Fund kwa
msaada mkubwa wa fedha na helkopta, pia Frunkfurt ,TANAPA na taasisi ya
utafiti wa wanyamapori(TAWIRI)"alisema.
HIfadhi ya Taifa ya Serengeti ni moja ya maeneo yenye Faru wengi kwa sasa hapa nchini kutokana na kuimarishwa ulinzi.
Post a Comment