PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MANYARA FC MABINGWA MICHUANO YA CHEMCHEM CUP 2018 NA KUJINYAKULIA MILION 1.7
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mgeni rasmi akikabidhi zawadi wa jezi kwa mabingwa wa chemchem cup 2018 timu ya Manyara fc Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mn...


Mgeni rasmi akikabidhi zawadi wa jezi kwa mabingwa wa chemchem cup 2018 timu ya Manyara fc

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akikagua timu ya Manyara fc kabla ya mchezo kuanza
Baadhi ya mashabiki wakishuhudia fainali ya mchezo huo

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti akikabidhi kikombe kwa washindi wa miochuano hiyo timu ya manyara fc mara baada ya kuibukana ushindi wa goli mbili kwa bila

Mfungaji bora wa mashindano hayo akibebwa na kushangiliwa kwa furaha na mashabiki wa Manyara fc


Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Manyara Mnyeti akikabidhi zawadi ya jezi kwa washindi wa pili wa michuono hiyo ambao pia wamejipatia kitita cha shilingi milioni 1.1

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti  akikagua timu zilizoingia fainalilya michuano ya chemchem cup 2018

Mwandishi wetu,Manyara

Timu ya soka ya Manyara FC imetwaa ubingwa wa michuano ya kupiga vita ujangili ya  Chemchem 2018, baada ya kuichapa timu ya majita FC  magoli 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa Chemchem, kijiji cha Mdori wilayani Babati,mkoa wa Manyara.

Katika mchezo huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa Manyara, Alexander Mnyeti magoli yote ya Manyara yalifungwa na Laurence  Michael Dk ya3 na 87 huku goLi pekee la Majita likifungwa na Hassan Hamza dk ya 90.

Kutokana na ushindi huo, Manyara FC walikabidhiwa zawadi ya fedha taslimu kiasi cha sh  1.7 milioni, kikombe chenye thamani ya sh 500,000 na mpira na seti ya jezi.huku Majita wakikabidhiwa fedha taslim 1.1 milioni, seti za jezi na mpira.

Kabla ya mchezo huo wa fainali, waliokuwa mabingwa watetezi, Mdori FC walifanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga kwa penati 4-3 timu ya Kalmaji baada ya kushindwa  kupata mbabe dakika 90 na kuvuta sh 700,000 na setiya jezi huku Kalmaji wakipata 300,000.

Akizungumza wakati akitoa zawadi, Mnyeti alipongeza taasisi ya Chemchem iliyowekeza hoteli za kitalii katika eneo hilo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya burunge kwa kuanzisha ligi hiyo tangu mwaka 2014.

Alisema michezo hiyo, imekuwa na faida kwani imehamasisha  vita dhidi ya ujangili, utunzwaji wa mazingira lakini pia imeibua vipaji vya vijana na kujenga afya zao.

"kutokana na mafanikio makubwa ya ligi hii ya Chemchem sasa nataka kuanza ligi ya mkoa wa Manyara na kamati hii ya chem chem itasimamia kwa kushirikiana na chama cha soka mkoa Manyara"alisema

Mkurugenzi wa Chemchem Foundation, Riccardo Tossi,alisema michuano hiyo ambayo imeshirikisha vijiji zaidi ya 10 vinavyozunguka burunge WMA, ambayo inapakana na hifadhi za taifa za Tarangire na Manyara.

"michuano hii imetumia zaidi ya sh 35 milioni na imefanikiwa sana kurejesha mahusiano mazuri baina yetu na wananchi lakini pia kusaidia vita dhidi ya ujangili.

Katibu wa mashindano hayo,  John Bura alisema jumla ya timu 20 za soka zilishiriki na timu tatu za wanawake, ambapo timu zote zilipewa seti za jezi na mipira.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top