PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MOBISOL YASHIRIKI SIKU YA USAFI WA MAZINGIRA DUNIANI, WAHIMIZA MATUMIZI YA NISHATI JUA KUTUNZA MAZINGIRA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Baadhi ya wafanyakazi wa Mobisol Wakifanya usafi wa mazingira jijini Arusha mapema leo Baadhi ya wafanyakazi wa Mobisol Wakifanya usa...
Baadhi ya wafanyakazi wa Mobisol Wakifanya usafi wa mazingira jijini Arusha mapema leo

Baadhi ya wafanyakazi wa Mobisol Wakifanya usafi wa mazingira jijini Arusha mapema leo


 Mwandishi wetu, Arusha.
Wakazi wa mkoa wa Arusha, wametakiwa kutumia nishati mbadala ya nguvu za jua, ili kujiepusha na uchafu na  uharibifu wa mazingira katika maeneo yao.

Mkuu wa kitengo cha masoko wa kampuni ya kimataifa ya Mobisol ,Seth Mathemu alitoa wito huo katika maadhimisho ya siku ya usafi wa mazingira  duniani, ambayo wafanyakazi wa kampuni hiyo, waliadhimisha katika jiji la Arusha kwa kufanya usafi.

Mathemu alisema matumizi ya nishati mbadala yanaweza kusaidia sana, kupambana na tatizo la uharibifu na uchafuzi wa  mazingira katika maeneo mbali mbali nchini.

"Suala la ulinzi wa mazingira na afya za watu ni sehemu ya malengo makuu ya kampuni ya Mobisol  imeungana na mataifa 156 duniani kushiriki katika maadhimisho ya usafi wa mazingira na kutoa misaada mbali mbali"alisema

Alisema Mobisol hadi sasa imeweza kuwaunganishia watu 500,000  umeme wa jua  katika nchi za Afrika ya Mashariki.

Awali Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega 
akizungumza katika maadhimisho hayo,alisema suala la usafi  na uhifadhi wa mazingira linapaswa kuwa la kudumu hapa nchini.

Alisema mkoa wa Arusha, umejipanga kuhakikisha unaendelea kuhifadhi mazingira na hivyo suala la usafi litaendelea kuwa la kudumu.

Katika kuadhimisha siku ya mazingira wafanyakazi wa kampuni ya Mobisol na baadhi ya wakazi wa jiji walishiriki usafi wa mazingira katika maeneo ya Ngarenaro, Njiro na Kisongo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top